Kundi la Halkojeni

Halkojeni ni elementi sita za kundi la 16 katika mfumo radidia au jedwali ya elementi.

Halkojeni

Tabia za pamoja hariri

Jina latokana na maneno mawili ya Kigiriki („Χαλκός“ = shaba, mtapo + „γεννώ“ = kuzaa, kufanya) na lamaanisha "fanya mtapo". Hii imetaja tabia ya kumenyuka haraka na metali hivyo kuunda kampaundi za kimetali. Halkojeni zote zina elektroni sita katika mizingo elektroni wa nje. Tabia hii huzisababisha kutafuta elektroni mbili za nyongeza kuwa hali tahibi ya elektroni nane kwenye mzingo wa nje na kuwa ioni ya chaji hasi thabiti.

Elementi hariri

Elementi hizi ni pamoja na oksijeni (O), kibiriti (S), seleni (Se), teluri (Te), poloni (Po) na elementi sintetiki ya ununheksi (Uuh).

O na S ni simetali, Po, Se na Te ni metaolidi na nusuvipitisho, lakini Se na Te vina pia umbo ambako huitwa metali tu. Uuh imetengenezwa mara mbili tu katika maabara kwa muda usiofika hata sekunde.