Ununheksi
Ununhexi ni elementi sintetiki yenye namba atomia 116 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 289 - 302. Alama yake ni Uuh. Si rahisi kutaja tabia zalke kwa sababu imetengenezwa mara mbili tu katika maabara kama atomi moja-moja.
Ununheksi (ununhexium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Ununheksi (ununhexium) |
Alama | Uuh |
Namba atomia | 116 |
Mfululizo safu | huaminiwa kuwa metali |
Uzani atomia | 289 - 302 g/cm³ (kadirio) |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 18, 6 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Asilimia za ganda la dunia | 0% (elementi sintetiki) |
Hali maada | mango |
Mengineyo | Ununheksi ni elementi sintetiki yenye nusumaisha mafupi sana iliyotengenezwa mara mbili tu |
Jina
haririJina latokana na maneno ya kilatini kwa "1" (unum) na kigiriki kwa "6" (heksa). Un-un-heksi yamaanisha hivyo moja-moja-sita yaani namba atomia ya elementi. Ununheksi ni jina la muda inawezekana ya kwamba jina lingine litatolewa kama wataaalamu hukubaliana.
Ufumbuzi
haririElementi iliwahi kutabiriwa na wanasayansi kuwa inaweza kupatikana. Ilitengenezwa mara mbili katika maabara ya taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Dubna (Urusi) kwa kuunganisha kiini atomia kimoja cha Kalsi na kiini kimoja cha Curi.
Nusumaisha yake ni fupi sana: haikudumu hata milisekunde.
Matumizi
haririKama elementi zote za sintetiki haina matumizi bado zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu.
Viungo vya Nje
hariri- WebElements.com - Uuh
- Apsidium - Ununhexium Ilihifadhiwa 17 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Second postcard from the island of stability Ilihifadhiwa 5 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ununheksi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |