Kungutana
Kungutana ni neno la Kisambaa linaloundwa na maneno mawili, kungu na tana. Kungu maana yake ni mwamba na tana maana yake ni zuri au jema. Maneno haya mawili yakiungana kunapatikana neno Kungutana ambalo maana yake ni mwamba mwema au mwamba mzuri.
Kungutana lilikuwa jina la kijiji cha kwanza kabisa cha Bumbuli, Tanzania; katika eneo hili kuna mwamba mkubwa sana na ndiyo maana pakapewa jina hilo la Kungutana yaani mwamba mwema. Eneo hilo lipo mpaka sasa na ndipo lilipojengwa kanisa kubwa la kwanza la Kilutheri na Wajerumani na shule ya Bumbuli Tanzania.
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kungutana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |