Kunyanyua vyuma
Kunyanyua vyuma ni moja ya mazoezi maarufu kwa ajili ya kujenga nguvu na kukuza mifupa. Mazoezi ya aina hii hufanywa kwa kunyanyua vyuma vyenye uzito wa aina mbalimbali.
Michezo mbalimbali duniani hutumia aina hii ya mazoezi kuimarisha nguvu na afya za wachezaji. Michezo hii ni kama vile mpira wa kikapu, mpira wa miguu, mpira wa magongo, riadha, mieleka, n.k.
Pia ni mchezo mmojawapo ambao toka zamani unafanyika katika Olimpiki.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kunyanyua vyuma kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |