Lüneburg ni mji wa Saksonia Chini nchini Ujerumani ya Kaskazini. Idadi ya wakazi wake ni takriban 72.800. Ni makao makuu ya wilaya ya Lüneburg; hadi kufutwa kwa mikoa ya Saksonia Chini ilikuwa pia makao makuu ya mkoa.

Sehemu ya mji wa Lüneburg








Lüneburg

Nembo
Nchi Ujerumani
Jimbo Saksonia Chini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 72.800
Tovuti:  http://www.lueneburg.de/

Lüneburg ni mji wa kihistoria. Nyumba nyingi za kale zimetunzwa zilizojengwa tangu karne ya 16. Tangu karne za zama za kati mji ulikuwa tajiri kutokana na chumvi iliyopatikana hapa chini ya ardhi yake na kufanyiwa biashara na sehemu za pwani la Bahari Baltiki na Bahari ya Kaskazini ambako chumvi ilitafutwa kwa ajili ya samaki zilizovuliwa kule. Samaki zilihifadhiwa katika chumvi na kuuzwa kote barani. Kwa njia hii mji ulikuwa tajiri ukapokelewa katika shirikisho la miji ya Hanse na kushindana na Hamburg juu ya kipaumbele katika sehemu hii ya Ujerumani. Tangu karne ya 17 biashara yake ilipungua na mji ulirudi nyuma.

Siku hizi ni mji wa wastani uliopo kando la rundiko la jiji la Hamburg takriban kilomita 50 upande wa kusini mashariki wa jiji hilo. Hakuna viwanda vikubwa lakini makampuni mengi madogo na ya wastani. Watu wengi wanapata ajira katika utumishi wa umma kwa sababu mji ni kitovu kwa ajili ya mahakama mbalimbali, kituo cha jeshi na idara mbalimbali. Chuo Kikuu kilizishwa mjini tangu mwaka 1989. Utalii uanleta wageni wengi wanataka kuangalia mji wa kihistoria na mazingira yenye misitu mingi na eneo maarufu la nyika ya Lüneburg.


Tazama pia

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lüneburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.