Bahari ya Kaskazini
Bahari ya Kaskazini ni tofauti na Bahari ya Aktiki, ambayo iko kaskaini zaidi
Bahari ya Kaskazini ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya Skandinavia (Norway na Denmark) upande wa mashariki, Ujerumani na Uholanzi upande wa kusini na Britania kwa magharibi.
Inaunganishwa na Atlantiki kwa njia ya Mfereji wa Kiingereza upande wa kusini na Bahari ya Norwei upande wa kaskazini.
Mlango wa bahari ya Skagerak unaiunganisha na bahari ya Baltiki. Mfereji wa Kiel unafupisha njia hii ukikata jimbo la Schleswig-Holstein ya Ujerumani. Kusini-magharibi kuna mlango wa Mfereji wa Kiingereza kati ya Britania na Ufaransa.
Kimo cha wastani ni mita 94 pekee.
Mito mikubwa inayoingia katika Bahari ya Kaskazini ni pamoja na Rhine, Elbe, Weser, Ems, Meuse, Schelde, Thames na Humber.
Bandari kubwa ni Rotterdam, Hamburg, Bremen na Antwerpen. Bahari ya Kaskazini ni kati ya bahari zinazopitiwa na meli nyingi duniani; zaidi ya robo ya usafiri wote wa baharini wa dunia unatokea hapo.
Katika sehemu za kaskazini kuna gesi na mafuta.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |