Landslide (Heroes)
"Landslide" ni sehemu ya ishirini na mbili ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Ni sehemu ya pili ya vipande vitatu vya mwisho katika msimu wa kwanza.[1]
"Landslide" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
"Boom." | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 1 Sehemu 22 | ||||||
Imetungwa na | Jesse Alexander | ||||||
Imeongozwa na | Greg Beeman | ||||||
Tayarisho la | 122 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 14 Mei 2007 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
Hadithi
haririMuungano wa Claire na Mr. Bennet umekatishwa ghafula na Peter ambaye amefikia hatua ya hatari ya kutojiweza baada ya kufyonza uwezo wa Ted. Peter anamwambia Claire ajiandae kwa kile anacholazimika kufanya ili kumzuia, lakini wakati Claire anajiandaa kutoa silaha kutoka katika mkoba wake, Peter ana nguvu ya kudhibi hali ya uwezo mpya na kujizuia mwenyewe asilipuke.
Akiwa mwenye huzuni, Hiro anasikitishwa ukosefu wa imani yake na upanga wake uliovunjika, Ando bado anaendelea kujaribu kurudisha nafsi ya Hiro. Ando anatafuta namba za simu kwenye Kurasa za Njano ili kukarabati upanga. Hiro anamzingua Ando kuhusu yule ambaye anamtarajia kumpa kwenye kitabu cha kumbukumbu ili kusawazisha mambo ya katana wa karne za kale, lakini Ando kafanikiwa kumpata mhunzi wa upanga akitangaza na nembo ya Helix.
Tukirudi mtaani, Mr. Bennet na Claire hatimaye wamepata nafasi ya kulonga. Mr. Bennet ameshangazwa kugundua uhusiano baina ya Peter na Claire na kumwelezea bintiye kuhusu mpango wake wa kuangamiza chombo cha ufuatiliaji na hivyo wataweza kuishi maisha yao ya kawaida tena; Claire anafikiria maisha ya kawaida haiwezekani, anatoa mazungumzo juu ya hali isiyo-ya-kawaida ya mpango wao, na kumweleza Bennet kwamba Peter huenda akawa na kitu cha "kuokoa dunia".
Wakati Peter anamshawishi Ted kwamba wawili hao wanastahili waondoke mjini New York City kabla hawajasababisha mlipuko, Mr. Bennet na[Matt Parkman|Parkman]] wanaendelea kutafuta chombo cha ufuatilizi. Claire, anaamini kwamba hii huenda ikawa ndiyo hatma yake, anaamua kuungana na Peter na Ted. Konani bila kutarajia mdukizi mwenye nguvu za kusikia majadiliano ya mbali: Sylar, ambaye ametambua mpango wa Peter wa kuondoka jijini, na kutazama nafasi ya kuendeleza zaidi mpango wake.
Marejeo
hariri- ↑ Lee, Patrick (2007-03-19). "Heroes Finale Details Leaked". SciFi Wire. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-22. Iliwekwa mnamo 2007-03-19.
Viungo vya Nje
hariri- Beaming Beeman: Episode 22: Landslide, Director's blog on the filming of this episode.