Lango:Hip hop/Wasifu uliochaguliwa/Dr. Dre


Dre akiwa katika tamasha fulani mnamo 2008
Dre akiwa katika tamasha fulani mnamo 2008

Andre Romelle Young (amezaliwa tar. 18 Februari, 1965) ni mtayarishaji wa rekodi, rapa, na mmiliki wa studio ya rekodi za muizki kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Dr. Dre. Dre ni mwanzilishi na mmiliki wa sasa Aftermath Entertainment na mmiliki mshiriki-msanii wa zamani wa studio ya Death Row Records, na pia kutayarisha albamu kadhaa kwa ajili yake na wasanii wengine kadhaa wa rekodi hiyo kama vile Snoop Dogg na Eminem.

Akiwa kama mtayarishaji, amejipatia sifa sana kwa kuukuza muziki wa West Coast G-funk, staili ya muziki wa rap unaotengenezwa na synthesizer-yenye ya taratibu, na mdundo wa nguvu.

Dr. Dre alianza shughuli za muiki akiwa kama mmoja kati ya wanamchama wa kundi la muziki la World Class Wreckin' Cru na kisha baadaye akaanzisha kundi lenye athira kubwa ya gangsta rap la N.W.A, ambayo ilivuma sana kwa mashairi yake mazito yenye kutaja maisha ya kiharifu na mtaani kwa ujumla. Mnamo mwaka wa 1992, alitoa albamu kama msanii wa kujitegemea. Na albamu ilikwenda kwa jina la The Chronic, ilitolewa ikiwa chini ya Death Row Records, na kumpelekea kuwa mmoja katia ya wasanii waliouza rekodi bora za muziki wa Marekani kwa mwaka wa 1993 na kushinda Tuzo ya Grammy kwa ajili ya single ya "Let Me Ride".

Soma zaidi....