Lango:Kenya/Picha nzuri/5
Boma la Yesu (Forte Jesus de Mombaça) ni ngome la kale mjini Mombasa (Kenya). Lilijengwa mwaka 1591 na msanifu Giovanni Battista Cairato kwa niaba ya Mfalme Philio Wareno. Ngome iko kwenye kisiwa cha Mombasa ikitazama mlango wa bandari ya kale.
Ilikuwa kituo muhimu cha Wareno kwenye njia ya mawasiliano kati ya Ureno na Uhindi.