Laurence Fishburne

Laurence John Fishburne III (amezaliwa tar. 30 Julai 1961) ni mshindi wa tuzo ya Academy na ya Emmy-mwigizaji, mtayarishaji, mwongozaji na mwandikaji bora script wa Kimarekani. Fishburne alianza kujibebea umaarufu tangu mwaka 1979 baada ya kuigiza filamu ya Apocalypse Now, vilevile katika Fled, Deep Cover , Boyz N the Hood, Teenage Mutant Ninja Turtles na mfululizo wa filazmu za Matrix.

Laurence Fishburne
Laurence Fishburne mnamo Septemba 2009
Laurence Fishburne mnamo Septemba 2009
Jina la kuzaliwa Laurence John Fishburne III
Alizaliwa 30 Julai 1961
Marekani
Jina lingine Lawrence Fishburne
Larry Fishburne
Kazi yake Mwigizaji
Mtayarishaji
Mwongozaji
Miaka ya kazi 1973 - mpaka leo
Ndoa Gina Torres (2002-yupo hadi sasa)

Hajna Moss (m. 1985)

Tovuti Rasmi Ya Lawarence Fishburne

Wasifu hariri

Maisha ya awali hariri

Fishburne alizaliwa mjini Augusta, Georgia, mamake alikuwa mwalimu wa sayansi na hesabu, na babake alikuwa ofisa wa umoja wa vijana. Wazazi wake walitalikiana akiwa bado bwana mdogo na yeye akachukuliwa na mamake na kwenda kuishi mjini Brooklyn, New York ambapo huko ndiko aliko kulia. Akiwa huko babake akawa anaenda kumwangalia mwanae mara moja kwa mwezi. Fishburne alipata elimu yake katika shule ya Lincoln Square Academy ya mjini New York ambayo baadae ilifungwa mnamo miaka ya 1980.

Maisha binafsi hariri

Fishburne amemwoa Hajna Moss mnamo mwaka 1985, nchini Ethiopia. Kwa pamoja wakazaa watoto wawili: wakiume, Langston, aliz. 1987, na wakike, Montana, aliz. mnamo 1991. Fishburne na Moss wakajakutarikiana kunako miaka ya 1990. Mke wa sasa wa Fishburne ni mwigizaji mwenzake filamu bi. Gina Torres, ambaye walioana mnamo tarehe 20 ya mwezi wa Septemba mwaka wa 2002. Kwa pamoja wana mtoto mmoja wa kike aitwaye Ashley, alizaliwa mwezi Juni mwaka 2007. Fishburne ni mshabiki mkubwa wa Paulo Coelho na wamepanga kuigiza filamu inayotokana na kitabu cha hadithi cha The Alchemist.

Fishburne pia ni balozi wa kujitolea wa UNICEF kwa Marekani.

Filamu alizoigiza hariri

  • One Life to Live (1973-1976)
  • Cornbread, Earl and Me (1975)
  • Fast Break (1979)
  • Apocalypse Now (1979)
  • Willie & Phil (1980)
  • Death Wish II (1982)
  • Rumble Fish (1983)
  • For Us the Living: The Medgar Evers Story (1983)
  • The Cotton Club (1984)
  • The Color Purple (1985)
  • Quicksilver (1986)
  • Band of the Hand (1986)
  • Pee-wee's Playhouse – Toleo la. 1-8 (1987)
  • A Nightmare on Elm Street 3: Dream Warriors (1987)
  • Gardens of Stone (1987)
  • Cherry 2000 (1987)
  • Red Heat (1988)
  • School Daze (1988)
  • Cadence (1990)
  • King of New York (1990)
  • Decoration Day (1990)
  • Class Action (1991)
  • Boyz N the Hood (1991)
  • Deep Cover (1992)
  • What's Love Got to Do with It? (1993)
  • Searching for Bobby Fischer (1993)
  • Higher Learning (1994)
  • Alien Warrior (1994)
  • Othello (1995)
  • Just Cause (1995)
  • Bad Company (1995)
  • The Tuskegee Airmen (1996)
  • Fled (1996)
  • Miss Evers' Boys (1997)
  • Hoodlum (1997)
  • Event Horizon (1997)
  • Always Outnumbered (1998)
  • The Matrix (1999)
  • Rugrats1991-
  • Once in the Life (2000)
  • Michael Jordan to the Max (2000)
  • Osmosis Jones (2001)
  • Deep Cover / Chill Factor (2001)
  • Biker Boyz (2003)
  • The Matrix Reloaded (2003)
  • Mystic River (2003)
  • The Matrix Revolutions (2003)
  • Assault on Precinct 13 (2005)
  • True Crime: New York City (Video Game, 2005)
  • Five Fingers (2006)
  • Akeelah and the Bee (2006)
  • Mission: Impossible III (2006)
  • Bobby (2006)
  • The Death and Life of Bobby Z (2007)
  • Teenage Mutant Ninja Turtles (2007)
  • Fantastic Four: Rise of the Silver Surfer (2007)
  • Black Water Transit (2007)
  • 21 (2008)
  • Days of Wrath (2008)
  • Tortured (2008)
  • 4Chosen (2008)
  • The Last Full Measure (2009)
  • The Alchemist (2009)

Filamu alizotayarisha hariri

  • TriBeCa (1993)
  • Hoodlum (1997)
  • Once in the Life (2000)
  • Akeelah and the Bee (2006)

Fila alizoandika script hariri

Once in the Life (2000)

Marejeo hariri

  1. http://www.britannica.com/eb/article-9399809/Laurence-Fishburne
  2. http://www.filmreference.com/film/15/Laurence-Fishburne.html
  3. http://movies.yahoo.com/movie/contributor/1800015265/bio Archived 6 Februari 2010 at the Wayback Machine.
  4. http://www.unicefusa.org/site/apps/nl/content3.asp?c=duLRI8O0H&b=46279&ct=3574749 Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje hariri