Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Georgia (maana) Georgia ni nchi iliyoko kati ya Ulaya ya Mashariki na Asia ya Magharibi. Ni sehemu ya eneo la Kaukazi, ikipakana na Bahari Nyeusi upande wa magharibi, Urusi upande wa kaskazini na kaskazini-mashariki, Uturuki upande wa kusini-magharibi, Armenia upande wa kusini, na Azerbaijan upande wa kusini-mashariki.

Georgia
საქართველო (geo)
Wito: ძალა ერთობაშია(Kigeorgia)
"Nguvu ni Umoja"
Wimbo wa taifa: Tavisupleba ("Uhuru")
Eneo la Georgia katika ramani ya Dunia
Eneo la Georgia katika ramani ya Dunia
Eneo la Georgia katika ramani ya Dunia
Mji Mkuu
and largest city
Tbilisi
41°43′N 44°47′E / 41.717°N 44.783°E / 41.717; 44.783
Official languages Kigeorgia (pia Kiabkhazi katika Abkhazia)
Government Jamhuri
Chanzo cha Taifa
Idadi ya watu
 -  2017 Makisio 3,718,200[1] (ya 1311)
 -  2014 Sensa 3,729,635
Pato la Taifa PPP
 -  Jumla $35.91
 -  Per capita $3,400
HDI (2022)0.814
very high ·60th
Currency Lari (ლ) (GEL)
Saa za eneo Moscow Time (MSK) (UTC+3)
 -  Summer (DST) Moscow Summer Time (MSD) (UTC+4)
Calling code 995
Patron saint Mt. George, Bikira Mariamu
Internet TLD .ge
1 Population figure excludes Abkhazia and South Ossetia.

Georgia inachukua eneo la kilomita za mraba 69,700 (maili za mraba 26,900). Ina idadi ya watu milioni 3.7, ambapo zaidi ya theluthi moja wanaishi katika mji mkuu na mji mkubwa zaidi, Tbilisi. Wenyeji wa Georgia, ambao ni asili ya eneo hilo, wanaunda sehemu kubwa ya idadi ya watu wa nchi hiyo na ndio taifa kuu.

Jiografia

hariri

Georgia ni nchi ya milima inayofikia kimo cha mita 5,068. Kati ya safu mbili za milima kuna tambarare ya Kolkhis.

Upande wa magharibi unafaidika zaidi na Bahari Nyeusi, hivyo una hali ya hewa safi na mvua nyingi inayofaa kwa kilimo hasa cha mizabibu.

Historia

hariri

Georgia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti lakini imekuwa nchi huru tangu 1991.

Maeneo ya Abkhazia na Ossetia ya Kusini yamedai uhuru pia na kwa sasa hayapo chini ya serikali kuu, lakini hayatambuliki kimataifa.

Utamaduni

hariri

Wakazi walio wengi (71%) huzungumza lugha ya Kigeorgia lakini kuna vikundi vya wazungumzaji wa Kirusi (9%), Kiarmenia (7%), Kiazeri (6%) na lugha nyingine.

Wageorgia wengi ni Wakristo wanaofuata Kanisa la Kiorthodoksi la Georgia (83.9%). Kuna pia wafuasi wa Kanisa la Kitume la Armenia (3.9%) na Wakatoliki (0.8%). Waislamu ni 9.9%, wakati Wayahudi wanazidi kuhama.

Watu maarufu

hariri

Mgeorgia anayejulikana zaidi duniani alikuwa Josef Stalin, mtawala wa Urusi wakati wa Ukomunisti.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Number of Population as of January 1, 2017 — National Statistics Office of Georgia" (PDF). Retrieved 1 May 2017.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
News media
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.