Leah Mwendamseka
Leah Richard Mwendamseke (maarufu kama Lamata; alizaliwa jijini Mbeya) ni mwigizaji mwongozaji na mwandishi wa filamu pamoja na tamthilia kutoka nchini Tanzania.
Lamata | |
---|---|
Faili:Lamataleah-20210416-0001.jpg | |
Amezaliwa | Leah Richard Mwendamseke Mbeya |
Jina lingine | Leah Lamata |
Miaka ya kazi | 2009-hadi sasa |
Ndoa | hajaolewa |
Lamata amejipatia umaarufu kutokana na kazi zake akifanya kazi na nyota wa filamu kama vile Jackline Wolper na Jennifer Kyaka. Huku tamthilia ya Kapuni na Jua Kali ikimpa umaarufu zaidi.
Maisha ya awali
Lamata alipata elimu yake katika shule ya msingi Ikuti kuanzia darasa la kwanza hadi la tano. Alimaliza elimu yake ya msingi katika shule iitwayo Kalobe shule ya Msingi ambapo alisoma kuanzia darasa la sita mpaka darasa la saba.[1]
Alisoma elimu yake ya sekondari katika shule ya Arage kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha pili, na kuhamishiwa katika shule ya Wanging’ombe Mkoani Iringa. Alimaliza masomo yake ya kidato cha tano na sita katika shule ya Perfect vision.
Maisha yake kwenye filamu
- 2008 Lamata alianza rasmi maisha ya uigizaji mwaka 2008, akianzia kikundi cha sanaa kilichojulikana kama Amka [2]. Akiwa na kundi hilo alianza kama muigizaji katika mchezo wa kuigiza wa Ndoano, uliorushwa na kituo cha Televisheni cha ITV
Mwaka huo huo alianza kuandika miswada ya filamu.
- 2009 Mwaka huu alianza kazi katika kampuni ya RJ chini ya uongozi wa Mwongozaji Ray Kigosi kama meneja wa uzalishaji. Alianza kujifunza kazi ya Uongozaji wa filamu akiwa na kampuni hiyo ya RJ. Amewahi kukiri kusaidiwa na watu katika kujifunza kazi hiyo ya Uongozaji filamu; watu hao ni pamoja na Vicent Kigosi,Selles Mapunda na Adam Kuambiana, lakini Vicent Kigosi ndiye alikua msaada mkubwa.
Mwaka 2023 alizindua rasmi kampuni yake iitwayo Lamata village of Entertainment
Tamthilia alizotayarisha
- Kapuni 2018-2019
- Jua Kali 2021 hadi sasa
Baadhi ya filamu alizoongoza
- Kigodoro
- Gumzo
- Figo
- Majuto
- Shaymaa
- Nesi Selena
- Stella
- After Death
- My Princess
- Tikisa
- Mr & Mrs Sajuki
- Poor Minds
- Pain Killer
- Mr.Nobody
- Jelousy
- Witch Doctor
- I am Lost
- Lonely
- Pusi na Paku
- Family War
- Kashfa
- Chocolate
- Time After Time
- House Maid
- Mke Mwema
- Rude
- Loreen
- Mens Day Out
- Dunia Nyingine
- Confusion
- Aching Heart
- All About Love
- Life 2 Life
- The Avenger
- Last Minutes
Marejeo
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-09. Iliwekwa mnamo 2018-11-17.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-09. Iliwekwa mnamo 2018-11-17.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leah Mwendamseka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |