Lewis Hamilton
Sir Lewis Carl Davidson Hamilton (alizaliwa 7 Januari 1985) ni dereva wa mashindano ya magari kutoka nchini Uingereza, kwa sasa anashindana katika Mbio za Langalanga akiwa na kampuni ya Mercedes-Benz. Hamilton anashikilia rekodi ya kushinda mataji saba ya dereva bora wa msimu akiwa sawa na Michael Schumacher— na anashikilia rekodi ya dereva alieshinda mbio nyingi zaidi za Grand prix (105), nafasi tatu za juu (104) na nafasi kumi za juu (201).
Lewis Hamilton | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Lewis Carl Davidson Hamilton |
Amezaliwa | 7 Januari 1985[1] Uingereza |
Kazi yake | Dereva wa Mashindano ya Magari |
Akiwa amezaliwa na kukulia Stevenage, Hertfordshire, Hamilton alijiunga na program ya madereva wadogo iliyotolewa na McLaren mwaka 1998. Hii ilipelekea kuwa dereva wa McLaren katika Mbio za Langalanga kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, hii ilimfaka kuwa mtu wa kwanza mweusi kushiriki kama dereva katika mfululizo wa mashindano hayo. Katika msimu wake wa kwanza, Hamilton aliweka rekodi nyingi, alimaliza nafasi ya pili nyuma ya Kimi Räikkönen kwa tofauti ya alama moja. Katika mashindano ya mwaka 2008, alishinda taji lake la kwanza kwa namna ya kipekee, kwenye Grand prix ya Brazil, alifanikiwa kumpita dereva alikua anaongoza mbio hizo hatua ya mwisho kabisa, ushindi huu ulimfanya kuwa dereva mdogo kuliko wote kuwahi kushinda taji la Mbio za Langalanga kwa wakati ule. Baada ya msimu sita akiwa na McLaren, Hamilton alisign mkataba na kujiungana Mercedes mwaka 2013.
Mabadiliko ya sheria za engine ya magari yam waka 2014, yalikua ndo mwanzo wa mafanikio ya Hamilton, kipindi hicho alishinda mataji sita zaidi. Alishinda mataji mfulilozo mwaka 2014 na 2015, msimu ulikua na ushindani mkali kutoka kwa dereva mwenza Nico Rosberg. Kufuatia kustaafu kwa Rosberg mwaka 2016, Dereva wa kampuni ya Ferrari Sebastian Vettel akawa mshindani mkuu wa Hamilton kwa misimu miwili, ambapo Hamilton aliweza kushinda mataji mfululizo tena, mwaka 2017 na 2018. Taji lake la tat una la nne alipata mwaka 2019 na 2020 na kufanikiwa kufikia rekodi ya Schumacher ya mataji saba kwa dereva. Hamilton alivunja rekodi ya kushinda Grand prix 100 mwaka 2021. Ataondoka Mercedes na kujiunga na Ferrari kuanzia msimu wa 2025 na kuendelea,.
Hamilton anapewa sifa nyingi kwa kuendeleza lengo la Mbio za Langalanga kufuatia mashabiki wengi nje ya mchezo huo, kwa sehemu ikisababishwa na aina ya Maisha yake, pamoja na kuwa mkereketwa wa masuala ya mazingira na jamii na kufuatilia sana masuala ya muziki na fasheni. Amekua pia balozi wa kupinga ubaguzi wa rangi akiwa na lengo ya kusukuma ongezeko la watu wa rangi tofauti katika mashindano ya magari. Hamilton alitajwa katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kwenye jarida la 2020 la Time na alipewa heshima ya Knight mwaka 2021.
Maisha ya Utoto na Elimu
haririLewis Carl Davidson Hamilton alizaliwa 7 Januari 1 1985 huko Stevenage, Hertfordshire.[1] Baba yake, Anthony Hamilton, ana asili ya Grenada, na mama yake Carmen Larbalestier, anatokea Uingereza, mji wa Birmingham,[3] hii humfanya kuwa chotara[4] Wazazi wa Hamilton walitengenga akiwa na miaka miwili, aliishi na mama yake pamoja na dada zake wakambo wawili Samantha na Nicola, mpaka alipofikisha miaka kumi na miwili.[5] Baadaye Hamilton aliishi na baba yake, mama yake wa kambo, na kaka yake wa kambo Nicolas ambaye naye ni dereva wa mashindano ya magari.[6][7] Hamilton alilelewa kwenye dhehebu ya Kikatoliki.[8]
Akiwa na umri wa miaka mitano, baba yake alimnunulia gari la kuchezea linaloendeshwa kwa rimoti.[9] Mwaka uliofuatia, Hamilton alimaliza nafasi ya pili kwenye mashindano ya BRCA, mshindani wake akiwa ni mtu mzima.[10] Kwa kuwa Hamilton alikua ndio mtoto pekee mweusi kwenye klabu yao, alikutana na changamoto nyingi za ubaguzi wa rangi.[9][11] Akiwa na umri wa miaka sita, baba yake alimnunulia gari dogo maarufu kwa jina la go-kart, hii ilikua zawadi ya sikukuu ya Noeli, alimuahidi kumuunga mkono kwenye kazi yake ya mashindano ya magari, hii ni endapo angefanya vizuri shuleni.[12] Kama sehemu ya kumsaidia mtoto wake, Baba yake Hamilto aliacha kazi aliyokua anafanya kama Meneja wa kitengo cha Technolojia ya Habari na akaamua kuwa muunda magari, Hii ilimfanya mara nyingi kufanya kazi zaidi ya nne zikiwa ni pamoja na mtu wa mauzo, muosha viombo, na kazi ya kubandika mabango ya madalali,[13] wakati huo wote aliendelea kuhudhuria mashindano ya magari aliyoshiriki mwanae.[14] Baadaye, Baba yake Hamilto alifungua kampuni yake mwenyewe ya Teknolojia ya Mawasiliano.[15] Aliendea kuwa meneja wa Hamilton mpaka mwanzoni mwa mwaka 2010.[16][17]
Hamilton alisoma katika shule ya Saint John Henry Newman, hii ni shule ya Kikatoliki inayopatikana Stevenage.[18] Kutokana na uonevu aliokua akipata shuleni, Hamilton mwenyewe anakiri kwamba aliamua kujifunza mchezo wa karate, lengo likiwa ni kwa ajili ya kujilinda mwenyewe.[19] Kuna kipindi alizuiwa kwenda shule baada ya ksuingiziwa kumshambulia mwanafunzi mwenzake ambaye alipata majeruhi yaliyolazimu kupelekwa hospitali kwa matibabu.[20] Pamoja na kushiriki mashindano ya magari, Hamilton alicheza mpira wa miguu pia, alikua miongoni mwa wachezaje wa timu ya shule, huko alicheza pamoja na Ashley Young.[15] Akiwa ni mshabiki wa klabu ya Arsenal, Hamilton anakiri kwamba endapo asingejihusisha na mashindano ya magari, basi angekua mchezaji wa mpira wa miguu ama mchezo wa Kriketi, hii ni kwasababu alicheza michezo yote kwenye timu za shule.[21] Mnamo Februari 2001, alianza masomo kwenye chou cha Cambridge Arts and Sciences (CATS), iliopo Cambridge.[22]
Mashindano ya Magari Ujanani
haririMchezo wa Karting
haririHamilton alianza mchezo wa karting mwaka wa 1993, na kwa haraka alianza kushinda mashindano daraja la cadet.[23][24] Miaka miwili baadaye, alikiwa na mika kumi tu, aliweka rekodi ya kuwa dereva mwenye umri mdogo zaidi kushinda mashindano ya daraja la cadet la Uingereza. Mwaka huo huo, Hamilton alimtafuta bwana Ron Denis, aliekuwa bosi wa timu ya McLaren Formula One kuomba sahihi, baada ya salamu akamuambia: "Habari, mimi ni Lewis Hamilton. Nimeshinda Mashindano ya Uingereza na siku moja nataka kuendesha magari yako."[13] Dennis aliandika kwenye kitabu cha sahihi cha Hamilton: "Nipigie simu baada ya miaka tisa, tutapanga kitu wakati huo."[25]
Hamilton alipokuwa na miaka 12, Ladbrokes waliweka dau ya 40/1, kwamba Hamilton atashinda mbio za Langalanga kabla ya kufikisha miaka 23; mwingine alitabiri, kwa uwezekano wa 150/1, kwamba angeshinda Ubingwa wa Madereva wa Dunia kabla ya kufikisha miaka 25.[26] Kufuatia ushindi wake wa pili mfululizo kwenye mashindano ya Super One na Ubingwa wa Uingereza, mwaka wa 1998, Dennis alimuita Hamilton,[10] ili kumpa nafasi katika programu ya Madereva wadogo chini ya McLaren.[27] Mkataba huo ulijumuisha chaguo la nafasi hapo baadaye kwenye mashindano ya Mbio za Langalanga, ambayo ingemfanya Hamilton kuwa dereva mwenye umri mdogo zaidi kushiriki mashindano hayo, ambapo alifanikisha.[23]
Ni dereva bora, mwenye nguvu sana na ana umri wa miaka 16 tu. Ikiwa ataendelea hivi, nina hakika atafikia F1. Ni jambo la kipekee kumuona kijana wa umri wake akiwa kwenye mzingo. Anaonekana wazi kuwa na akili sahihi ya mashindano.
—Michael Schumacher, akizungumza kuhusu Hamilton mwaka 2001[28]
Hamilton aliendelea kupanda kwenye viwango vya Intercontinental A mwaka 1999, Formula A mwaka 2000, na Formula Super A mwaka 2001, na akawa Bingwa wa Ulaya mwaka 2000. Kwenye ngazi ya Formula A na Formula Super A, akiwa chini ya TeamMBM.com, dereva mwenzake alikuwa Nico Rosberg, ambaye baadaye aliechezea timu za |Williams na Mercedes ngazi ya Mbio za Langalanga; baadaye walishirikiana tena wakiwa na timu ya Mercedes kuanzia 2013 hadi 2016. Kufuatia mafanikio yake ya karting, Klabu ya Uingereza ya madereva wa mashindano ilimfanya kuwa mwanachama wa "Rising Star" mwaka 2000.[29] Mwaka wa 2001, Michael Schumacher aliamua kurudi kwenye mashindano ya karting na kushindana dhidi ya Hamilton pamoja na Vitantonio Liuzzi na Nico Rosberg madereva ambao baadae walikuja kushindana ngazi ya Mbio za Langalanga. Hamilton alimaliza wa saba kwenye fainali, nafasi nne nyuma ya Schumacher. Ingawa wawili hao walionana mara chache tu kwenye mzunguko, Schumacher alimpongeza kijana huyo kutokea nchini Uingereza.[30]
Formula Renault na Formula Three
haririHamilton alianza safari yake ya kuendesha magari ya mashindano mwaka2001 katika mashindano ya Renault majira ya baridi ya nchini Uingereza, alimaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.[10] Hii ilimpelekea kushiriki mashindano ya Renault Championship ya mwaka 2002 akiwa na Manor Motorsport, ambapo alimaliza nafasi ya tano kwa ujumla.[31] Alibaki na Manor kwa mwaka mwingine, akishinda ubingwa mbele ya Alex Lloyd .[32] Baada ya kushinda ubingwa huo, Hamilton alikosa michezo miwili ya mwisho wa msimu ili kuanza kushiriki kwenye raundi ya mwisho ya Formula 3 Championship ya Uingereza.[33] Alitoka kwenye mashindano yake ya kwanza baada ya gurudumu lake kuchanika,[34] na mashindano ya pili alipata ajali kwa kugongana na mwenzake, iliopelekea kupelekwa hospitali.[35] Aliulizwa mnamo 2002 kuhusu matarajio ya kuwa mmoja wa madereva wadogo zaidi kwenye Mbio za Langalanga, Hamilton alijibu kuwa lengo lake "si kuwa mdogo zaidi katika Mbio za Langalanga" bali "kuwa na uzoefu kisha nionyeshe kile ninachoweza kufanya kwenye Mbio za Langalanga".[36] Alianza kushiriki na Manor msimu 2004 Formula 3 Euro Series, akimaliza mwaka akiwa wa tano kwenye msimamo wa ligi.[37] Pia alishinda Bahrain F3 Superprix,[38] na kushiriki mara mbili mbio za Macau.[39][40] Timu ya Williams ilikuwa karibu kumsaini Hamilton lakini hawakufanya hivyo kwa sababu BMW, wasambazaji wao wa injini wakati huo, hawakutaka kufadhili mkataba wake.[41] Hamilton mwishowe alisaini tena na McLaren. Kulingana na mtendaji wa McLaren wakati huo na baadaye kuwa Mkurugenzi Mtendaji Martin Whitmarsh, ambaye alihusika moja kwa moja katika kumlea Hamilton kupitia mpango wa timu ya madereva wachanga, yeye na baba yake Anthony Hamilton walipishana vikali mwishoni mwa msimu, huku baba yake akisisitiza kupanda hadi GP2 kwa 2005, ilhali Whitmarsh alihisi kuwa anapaswa kubaki Formula 3 kwa msimu wa pili. Mwishowe, Whitmarsh alivunja mkataba wa Hamilton; hata hivyo, Hamilton alimwita Whitmarsh wiki sita baadaye na kusaini tena na timu.[13] Hamilton aliendesha majaribio ya kwanza kwa McLaren mwishoni mwa 2004 katika Silverstone.[42] Hamilton alihamia kwa mabingwa wa Euro Series ASM kwa msimu wa 2005 na alitawala mashindano, akishinda mbio 15 kati ya 20.[10] Pia alishinda Marlboro Masters of Formula 3 katika Zandvoort.[43] Baada ya msimu, jarida la Uingereza Autosport lilimuweka katika toleo lao la "Dereva 50 Bora wa 2005", akimorodhesha Hamilton katika nafasi ya 24.[10]
GP2
haririHamilton alihamia ART Grand Prix ambayo ni timu dada wa ASM, kwa msimu wa 2006.[44] Hamilton alishinda ubingwa wa GP2 kwenye mashindano yake ya kwanza, akiwashinda Nelson Piquet Jr. na Alexandre Prémat.[45] Alipata ushindi mkubwa kwenye uwanja wa Nürburgring, licha ya adhabu ya mwendo kasi kwenye eneo la kufanya marekebisho ya magari.[46] Kwenye mashindano ya Silverstone, Hamilton aliwapita wapinzani wawili eneo la Becketts, sehemu yenye mfululizo wa kona kali za mwendokasi ambapo kumpita anayekutangulia huwa ni nadra.[47] Kwenye mbio za Istanbul, alishika nafasi ya pili akitokea nafasi ya kumi na nane alipodondokea baada ya kushindwa kumudu gari na kufanya lizunguruke.[48] Hamilton alishinda taji hilo katika hali isiyo ya kawaida, akinyakua pointi ya mzunguko wa kasi zaidi kutoka kwa Giorgio Pantano huko Monza.[49] Mafanikio ya Hamilton katika michuano ya GP2 yaliambatana na nafasi ya wazi McLaren baada ya kuondoka kwa Juan Pablo Montoya kwenda NASCAR na Kimi Raikkonen kwenda Ferrari.[50][51] Baada ya miezi kadhaa ya uvumi juu ya nani kati ya Hamilton, Pedro de la Rosa au Gary Paffett ataungana na bingwa mtetezi Fernando Alonso msimu wa 2007, Hamilton alithibitishwa kuwa dereva wa pili wa timu hiyo.[52] Alijulishwa uamuzi wa McLaren mwishoni mwa Septemba, lakini habari hiyo haikuwekwa wazi kwa karibu miezi miwili, kwa hofu kwamba ingefunikwa na tangazo la kustaafu kwa Michael Schumacher.[53]
Tanbihi
hariri- ↑ 1.0 1.1 Kelso, Paul. "Profile: Lewis Hamilton", The Guardian, 20 April 2007.
- ↑ Cary, Tom. "Anthony Hamilton's massive support makes parting with Lewis easier to understand", The Daily Telegraph, 3 March 2010. Kigezo:Cbignore
- ↑ "FreeBMD Entry Info". freebmd.org.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Being F1's first black driver is important". lewishamilton.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Machi 2018. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mathé, Charlotte (12 Julai 2014). "10 Things About ... Lewis Hamilton". Digital Spy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kigezo:Cite AV media
- ↑ Matt Dickinson. "Lewis Hamilton admits: 'I just don't know how I kept my cool'", The Times, 3 November 2008. Retrieved on 2024-10-01. Archived from the original on 2009-05-09.
- ↑ "Lewis Hamilton Biography – Trivia", The Biography Channel, London: thebiographychannel.co.uk. Retrieved on 2024-10-01. Archived from the original on 2014-05-25.
- ↑ 9.0 9.1 "BBC Radio 4 - Radio 4 in Four - Race to the top: Lewis Hamilton". bbc.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 10.0 10.1 10.2 10.3 10.4 "Lewis Hamilton Biography". F1Fanatic.co.uk. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Machi 2009. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Lewis Hamilton: I had a lot of bullying and racism at school". Eurosport (kwa Kiingereza). 25 Septemba 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Juni 2023. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kigezo:Cite magazine
- ↑ 13.0 13.1 13.2 Benson, Andrew. "Challenger, champion, change-maker: The real Lewis Hamilton story". bbc.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Novemba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Classen, Robin (22 Mei 2018). "'Thanks dad!' Lewis Hamilton reflects on his F1 championship journey". Wheels. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Februari 2019. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 15.0 15.1 Owen, Oliver. "The real deal", The Guardian, 3 June 2007.
- ↑ Callow, James. "Lewis Hamilton signs with Simon Fuller's XIX Entertainment", The Guardian, 14 March 2011.
- ↑ "Words from Lewis Hamilton's father inspired Hungarian Grand Prix pace, says Wolff | Formula 1®", 5 August 2019. (en)
- ↑ "Lewis Hamilton fact file". BBC Southern Counties. BBC. 19 Juni 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Desemba 2010. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Davies, Gareth A. "A salute to the real Lewis Hamilton", The Daily Telegraph, 5 July 2007. Kigezo:Cbignore
- ↑ Younge, Gary (10 Julai 2021). "Lewis Hamilton: 'Everything I'd suppressed came up – I had to speak out'". theguardian.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Lewis Hamilton: I could have been a footballer", The Daily Telegraph, 29 October 2007.
- ↑ Hamilton, Lewis (2007). Lewis Hamilton: My Story. HarperCollins. ISBN 978-0-00-727005-7.
- ↑ 23.0 23.1 "Hamilton's kart sells for £42,100", BBC News, 19 June 2007.
- ↑ Baker, Andrew. "Lewis Hamilton's karting days have helped him become one of F1's best drivers", The Daily Telegraph, 29 October 2008.
- ↑ "Teams target the next generation of stars", The Times, 17 June 2007. Retrieved on 2024-12-03. Archived from the original on 2008-12-04.
- ↑ Westcott, Kathryn. "The curious world of long-term bets", BBC News, 9 July 2012.
- ↑ Wolff, Alexander (12 Juni 2007). "Better Than Sex". Sports Illustrated. Associated Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2008. Iliwekwa mnamo 21 Agosti 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Schumacher Tips Hamilton for Future Glory", AtlasF1, 28 October 2001. Retrieved on 2024-12-03. Archived from the original on 2007-10-24.
- ↑ "Lewis Hamilton Biography". Vodafone McLaren Mercedes official website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Machi 2010. Iliwekwa mnamo 5 Julai 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "When Hamilton raced Schumacher". F1Fanatic.co.uk. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Oktoba 2007. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Formula Renault 2.0 UK 2002 standings". driverdb.com. Driver Database. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Formula Renault 2.0 UK 2003 standings". driverdb.com. Driver Database. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Septemba 2022. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "British Formula 3 Championship 2003 standings". driverdb.com. Driver Database. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Thomas, Stella-Maria. "Brands Hatch round 23 race report", Motorsport.com, 10 October 2003. Retrieved on 2024-12-04. Archived from the original on 2007-09-30.
- ↑ Thomas, Stella-Maria. "Brands Hatch round 24 race report", Motorsport.com, 13 October 2003. Retrieved on 2024-12-04. Archived from the original on 2007-09-27.
- ↑ Kigezo:Cite magazine
- ↑ "Formula 3 Euro Series 2004 standings". driverdb.com. Driver Database. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "1st Bahrain F3 Superprix 2004 Race".
- ↑ "Hamilton misses podium". Autosport. 16 Novemba 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Julai 2018. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Macau: Bad day for the Brits". Autosport. 21 Novemba 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Julai 2018. Iliwekwa mnamo 20 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Williams 'came close to Lewis deal'", ITV-F1.com, 2 March 2008.
- ↑ "New McLaren bad news for Wurz", crash.net, 16 December 2004.
- ↑ "Lewis Hamilton portrait", Formula 3 Euro Series, 28 August 2005.
- ↑ "Lewis Hamilton", Sky Sports, Sky, 10 February 2010.
- ↑ "2006 GP2 SERIES - Standings". motorsportmagazine.com. Motor Sport Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 19 Desemba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nurburgring 2006: Hamilton beats penalty and rest", crash.net, 6 May 2006.
- ↑ "Silverstone: DAMS team race two report", motorsport.com, 14 June 2006. Retrieved on 2024-12-04. Archived from the original on 2018-12-20.
- ↑ "Istanbul 2006: Zuber win overshadowed by Hamilton", crash.net, 27 August 2006.
- ↑ "GP2 Series – History". GP2 Series (official website). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Mei 2008. Iliwekwa mnamo 5 Julai 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "McLaren agree to release Montoya", BBC Sport, 11 July 2006.
- ↑ "Ferrari reveal Räikkönen signing", BBC Sport, 10 September 2006.
- ↑ "Hamilton gets 2007 McLaren drive", BBC Sport, 24 November 2006.
- ↑ Tremayne, David. "Hamilton's F1 drive is a dream come true", The Independent, 25 November 2006.
Viungo vya nje
hariri- Official website
- Lewis Hamilton biography at MercedesAMGF1.com
- Lewis Hamilton at the Internet Movie Database
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lewis Hamilton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |