Lords of the Underground

Kina Lords of the Underground (L.O.T.U.G.) ni kundi la muziki wa hip hop kutoka mjini Newark, New Jersey nchini Marekani. Kundi linaunganishwa na ma-MC watatu ambao ni Mr. Funke na DoItAll Dupré ambaye alikutana na DJ Lord Jazz (mwenyeji wa Cleveland) wote watatu walikutana wakati wanasoma katika Chuo Kikuu cha Shaw.

Lords of the Underground
Asili yake Newark, New Jersey
Aina ya muziki Hip hop
Miaka ya kazi 1990–1995
1999–hadi sasa
Studio Pendulum Records, Jersey Kidz Records
Wanachama wa sasa
DoItAll
Mr. Funke
DJ Lord Jazz

Kundi lilitoa albamu yao ya kwanza iliyoitwa jina la Here Come the Lords mnamo tar. 27 Septemba, 1993 huku suala la utayarishaji likishughulikiwa na Marley Marl na K-Def. Albamu ilishika nafasi ya 66 kwenye chati za Billboard 200 na imeingiza vibao vitano katika chati kadhaa nchini humo, ikiwa ni pamoja na kibao chao maarufu cha "Chief Rocka".

Kundi likaendelea kutoa albamu yao ya pili iliyoenda kwa jina la Keepers of the Funk kwa mwaka uliofuatia mnamo tar. 1 Novemba 1, 1994. Keepers of the Funk imefika kilele cha 47 kwenye chati za Billboard 200 na kuingiza vibao vikali vitatu katika chati kadhaa, kibao kilichotamba zaidi ni kile cha "Tic Toc". Kundi lilikufa mwaka wa 1995.

Mwaka wa 1999, kundi lilirudi tena uwanjani kwa kutoa albamu yao ya tatu iliyokwenda kwa jina la Resurrection. Ilitolewa kupitia studio ya Queen Latifah "Jersey Kidz", ilitolewa katika hali ya chini sana kiasi hata watu wengi wasijue kama albamu imetolewa. Mabwana walirudi tena mwaka wa 2007 kwa ajili ya albamu yao ya nne iliyoitwa House of Lords, lakini imekuwa kama ile ya Resurrection, imeanguka katika kufikia chati za Billboard.

Diskografia hariri

Albamu za Studio hariri

Mwaka Jina Nafasi ya Chat
U.S. U.S. R&B
1993 Here Come the Lords
  • Imetolewa: September 27, 1993
  • Studio: Pendulum
66 13
1994 Keepers of the Funk
  • Imetolewa: November 1, 1994
  • Studio: Pendulum
57 16
1999 Resurrection
  • Imetolewa: April 20, 1999
  • Studio: Jersey Kidz
2007 House of Lords
  • Imetolewa: August 21, 2007
  • Studio: Affluent

Singles hariri

Mwaka Single Chati Albamu
U.S. Hot 100 U.S. R&B U.S. Rap
1992 "Psycho" 17 Here Come the Lords
1993 "Chief Rocka" 55 35 1
"Funky Child" 74 52 2
"Here Come the Lords" 93 67 18
1994 "Flow On" 36
1994 "Tic Toc" 73 52 17 Keepers of the Funk
1995 "What I'm After" 42
"Faith" 49

Viungo vya Nje hariri