Louis Armstrong (4 Agosti 19016 Julai 1971) alifahamika zaidi kama mwanamuziki wa Kiamerika wa Jazz na mpuliza tarumbeta mahiri na aliye machachari.

Louis Armstrong

Louis alizaliwa katika jiji la New Orleans, Louisiana, alipewa jina la utani "Satchel Mouth" ambalo baadaye lilikuja kukatishwa kama "Satchmo". Maisha ya Louis utotoni mwake yalikuwa ya shida kwani alitumia muda mwingi bila maana na vijana wa mjini New Orleans. Hii ilitokana na baba yake William Armstrong kuitelekeza familia, hiyo ilimfanya Louis kuishi bila kuwa na baba. Hivyo alilelewa na mama yake Mary Albert Armstrong (1886-1942). Baada ya kufariki Mary, Louis na mdogo wake wa kike aliyeitwa Betrice Armstrong Collins (1903-1987) wakiwa chini ya uangalizi wa bibi yao Josephine, Louis kwanza alianza kujifunza kupiga koneti (hii ni aina ya tarumbeta dogo).

Ilikuwa ni tarumbeta yake ya kwanza kuinunua na ilitokana na pesa zake za mkopo alizopata kutoka kwa akina Karnofsky (hii ni jamii ya wahamiaji wenye asili ya Kiyahudi na Kirusi). Louis alipenda kusikiliza wanamuziki wa kizamani kila alipopata nafasi, alijifunza kutoka kwa Bunk Johnson, Buddy Petit na yote kuhusu Joe "King" Oliver ambaye alikuwa kama mshauri wake na aliyempa uzoefu na zaidi alimjenga kijana Louis. Louis baadaye alihudhuria brasi bendi zinazotumbuiza kwenye meli za mto Mississippi. Kwanza alianza kutembea na benndi ya The Wellregarded band iliyokuwa ikivinjari kwa meli kwenye mto wa Mississipi hiyo ilimfanya kutumia muda wake vizuri kama aliyekwenda chuo kikuu, na tangu hapo ilimpa uwezo na uzoefu wa kufanya kazi kwa kuziandika na kupanga mipango ya kazi zake, wakati Oliver alipoondoka New Oleans 1919, Louis alichukua nafasi yake kwenye bendi ya Kid Ory's band, hii ilikuwa ni bendi iliyokuwa kali na ya kiwango cha juu mjini hapo. 19 Machi,1918 Louis alimuowa Daisy Parker, huyu alitoka Gretua, Louisiana, walipata mtoto wa kulea wa miaka mitatu waliyemuita Clarence Armstrong, Daisy Parker hakuweza kudumu kwenye ndoa na Louis, hiyvo wakatengana mapema. Mwaka 1922 Louis alijiunga na Creole Jazz Band iliyo mjini Chicago baada ya kupata mualiko kutoka kwa Joe "King" Oliver hii ilikuwa ni bendi ya Oliver na iliyokuwa bora na kali mjini Chicago, mwanzoni mwa miaka ya 1920 katika wakati huo Chicago ilipokuwa makao ya Jazz. Louis alitoa rekodi zake za kwanza na wakati huo alikuwa akipuliza tarumbeta ya pili kwenye bendi ya Oliver mwaka 1923 Louis alifurahi kufanya kazi na Oliver lakini mke wake mwengine aliyekuwa mpiga piano Lil Hardin Armstrong alimfanya ajisikie kuwa mtu muhimu zaidi katika bendi hivyo Louis na Oliver wakatengana bila migongano hiyo ilkuwa ni mwaka 1924 Louis aliondoka nakuelekea jiji la New York kupiga na kundi la Fletcher Henderson Orchestra hii ilikuwa ni bendi bora ya Waamerika wenye asili ya Afrika kwa wakati huo. Louis alianza kupuliza tarumbeta kwa mitindo tofauti na mvuto wa aina yake akiwa na wanamuziki wengine kwenye nafasi yake na alimumbukiza aina ya upulizaji wake mpuliza saksi muongozaji Coleman Hawkins na hii utaweza kukubali au kukataa iwapo utasikiliza rekodi zilizopigwa na bendi hiyo kwa kipindi hicho, na toka wakati huo alitoa rekodi nyingi kwa kufanya mpango na rafiki zake wa zamani wa New Orleans kama mpiga piano Clarence Williams pia alishirikiana na waimba Blues na wapiga Jazz kama Duke Ellington, Louis alifariki kwa ugonjwa wa moyo tarehe 4 Julai 1971 akiwa na umri wa miaka 69.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Louis Armstrong kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.