Luciana Demingongo

Luciana Demingongo (alizaliwa 28 Februari 1960) ni mwanamuziki kutoka mjini Kinshasa-Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alifahamika sana miaka ya 1990 akiwa na kundi lake Nouvelle Generation lililovuma na albamu ya Vigilancy iliyotoka 1992.

Muziki na maisha

hariri

Alizaliwa kama mtoto pekee kwa jina la Luciana Litemo Demingongo mnao Februari 28, 1960 huko mjini Kisangani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa ushupavu wake, Luciana ameoa na kupata watoto sita.


Ikiwa kama sehemu ya kutangaza kazi yake ya muziki, ilimlazimu kuishi kati ya Paris na Brussels.

Mwaka wa 1977, wakati huo akiwa na umri wa miaka 17 pekee, kufuatia kuvunjika kwa kundi la muziki la MAQUIS EXPRESS SASA-BATA, ambapo wakati huo lilikuwa bora la tatu kwa mjini Kisangani, kundi jipya likazaliwa . Kundi hilo liliitwa SASA-MUSICA huku ndani kukiwa na bwana Luciana.

Kundi lilianza kwa kasi ya kimbunga huku Luciana akitumika kama kivutio kwa kuwa ni ingizo jipya. Ikawavuruga wale wanamuziki wa waliotangulia katika tasnia ya muziki wa dansi nchini Kongo.

Ndani ya mwaka mmoja, yakatokea mapunduzi makubwa katika muziki. Nyimbo zao zilipigwa katika redio ya taifa. Kundi likawa bora mjini Kisangani huku mwaka 1978 Luciana akichukua kama mtunzi bora kwa kibao chao cha Horizon. Pia amepata kushinda kuwa kama nyota bora wa Kisangani.

Mwaka wa 1979, akapasua kiwango cha kitaifa na kutua jijini Kinshasa akiwa na rafikize wawili Pépé Lusambo na Dicky Dikala. Lengo likiwa kuwavuta karibu wakazi wa Kinshasa kusikiliza kazi yake. Akiwa hapa, akaunda kundi lililodhaminiwa na Father Buffalo na José Makutu lakini mazingira ya mjini yalikuwa magumu mno licha ya kupata mialiko kadhaa huko Cabaret Liyoto, mji mdogo katikati ya jiji la Kinshasa.

Mwaka wa 1980, makundi kadhaa walimwita kwa minajili ya kurekodi naye. Makundi hayo ni pamoja Green Helmets akiwa na Pépé Felly Manuaku kwa ajili ya albamu zao. Boketshu akatumia fursa kwa ajili ya wimbo wake wa Ambochila (cfr.Volume 1 katika albamu ya vibao vikali ya Papa Wemba na Viva la musica). Kila Jumamosi, huwa zamu ya Papa Wemba na kundi lake la Viva la musica, Luciana alitumbuiza na kundi lake la CHIC CHIC MATONGE.

Lakini kwa sababu ya kiafya, mnamo mwaka wa 1981, alilazimika kurudi mjini Kisangani kujiunga na makundi mazito na kongwe ya mjini Kisangani. Kundi hilo ni SINGA MUAMBE la Bwana Gracia NDONGALA. Akapita zake hadi katika kundi la Guvano VANGU (zamani iliitwa Afrisa of Tabu Ley Rochereau) kisha Rubens (zamani iliitwa Vévé de Kiamuangana Mateta na of T.P.O.K.JAZZ ya Franco Luambo Makiadi).


Kupitia hao wazee, akajifunza muziki mpya wenye kueleweka. Mwaka huohuo wa 1981, akachaguliwa kama Mwimbaji Bora wa Muziki wa Zaire.

Wakati huo huko mjini Kinshasa, katika moja ya kundi maarufu jijini humo, mambo yanaliendea kombo kundi la Viva la Musica; King Kester Emeneya, Bipoli na Fulu na wengine wanaachana na Papa Wemba na kuanzisha kundi lao la Victoria Eleison.


Papa Wemba analazimika kujipanga upya kwa dutu mpya lakini muda huo Luciana hayupo tena mjini Kinshasa. Papa Wemba alimwomba mke wa Amazon, ambaye wakati huo alikuwa akitembelea mjini Kisangani akiwa na mdogo wake wa kike. Alimtaka afanye hakikisho anarudi Kinshasa akiwa na Le Rossignol Luciana.

Akiwa na Reddy Amisi, Maray Maray na Lidjo Kwempa, akafanya kazi yake ya kwanza iliyotukuka ndani ya Viva la Musica. Huku sauti yake ikiwakumbusha Wazaire sauti ya Gina wa Gina, binamu yake kutoka Cavacha zama za Zaïko Langa Langa. Jambo likalipuka na watu wa Kinshasa wakampenda.

Kwa zaidi ya miaka kumi alikuwa karibu sana Papa Wemba. Tangu 1987 alikuwa akiishi kati ya Ulaya  na Afrika, pia Brussels na Paris.

Ili kusonga mbele zaidi, mnamo 13 Oktoba, 1992, akiwa na baadhi ya rafikize hasa Fafa Maestro (Fafa de Molokai), Awilo Longomba, Djena Mandako, Fataki ya José, Lodjo Kwempa, Boss Matuta, Zola Collégien, na mpiga gitaa Bojack Bongo Wende, walitoka Viva la Musica na kuunda kundi la "THE NEW GENERATION" au kwa Kifaransa liliitwa "Nouvelle Generation."


Akatoa albamu yake ya kwanza akiwa kama msanii wa kujitegemea kwa mtindo wa Zimpompa-pompa. Kundi likatumbuiza Ulaya yote. Kwa hakika walileta ladha mpya ya muziki kwa wapenda muziki. Waliendelea kufanya hivyo hadi pale kidudu mtu alipoingia kwa dhamira ya kuwaangamiza.

Albamu alizotoa kati ya 1992-2009

hariri

1.  Luciana Et Nouvelle Generation De La Republique Democratique Du Congo - 1994

2.  Sang Bleu "Aziza" - 1996

3. Beauté Ya Mt - 1998

4. Feza - 1999

5. Pool Malebo - 2002

6. Rumba Lolango - 2004

7. Zanzibar - 2009

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Luciana Demingongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.