Lydia Lindeque

Mwigizaji wa Filamu wa Afrika Kusini

Lydia Lindeque (jina la kuzaliwa: Rachel Alida du Toit; 15 Januari 191616 Julai 1997) alikuwa mwigizaji tokea Afrika ya Kusini wa kabila la Makaburu.

Lydia Lindeque
Amezaliwa Rachel Alida du Toit
15 Januari 1916
Bendera ya Afrika Kusini Afrika Kusini
Amekufa 16 Julai 1997
Andorra
Jina lingine Alida du Toit
Kazi yake Mwigizaji
Ndoa John Mantel
Lydia Lindeque

Awali alijulikana katika jukwaa kwa jina Alida du Toit, Alianza ziara katika umri wa miaka kumi na saba na kampuni ya uigizaji iliyojulikana kama Paul de Groot's acting company. Mapema alirithi jina Lydia Lindeque, Alifanya kazi na mastaa mbalimbali wa zama katika miongi ifuatayo, ikiwemo Taubie Kushlick mwaka 1958. Kwa mara ya kwanza alifanya katika kiingereza mwaka 1943, katika William Shakespeare's Twelfth Night, na katika mwaka 1945, alisafiri kuelekea Misri na Italia kuongoza jukwaa la michezo la jeshi la waafrika weusi lililowekwa hapo. Aliolewa na mwandishi wa tamthilia Uys Krige mwaka 1937, baadae wakatengana na kuolewa na John Mantel. Baada ya kustaafu mwaka 1976, Alifariki huko Andorra mwaka 1997.

Maisha ya Familia

hariri

Lindeque aliolewa na Mwandishi wa tamthilia Uys Krige mwaka 1937. Walikuwa na watoto wawili, binti aliitwa Eulalia na wa kiume aliitwa Taillefer, walizaliwa 1937 na 1944. Hata hivyo familia ilikuwa na changamoto ya kipato. Walikuja kutengana wakati wa kuzaliwa mtoto wao mdogo na baadae akaolewa na John Mantel. Aliondoka Afrika kusini na Mantel na kustaafu kwenda Andorra mwaka 1976. Mnamo 16 Julai 1997 alifariki nyumbani kwao huko.

  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lydia Lindeque kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.