MGIMO
Chuo Kikuu cha Moskva cha Mahusiano ya Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi (Kirusi: Московский государственный институт международных отношений (Университет) МИД России MGIMO MID) ni chuo kikuu kimojawapo mjini Moskva katika Urusi.
Kimeanzishwa mwaka 1943 kikiwa ni kitivo cha Chuo Kikuu cha Taifa cha Moskva (Moscow State University - MSU), mwaka 1944 kikapata hadhi ya chuo kikuu.
Kwa sasa zaidi ya wanafunzi 4500 wanasoma huko, wakiwemo wageni. Jumla ya vitivo ni 12. Masomo yanayopewa ni pamoja na udiplomasia, uchumi wa dunia, uandishi habari, utembezi, sheria ya kimataifa n.k.
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi: http://www.mgimo.ru Archived 28 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
- Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi: http://www.mid.ru
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu MGIMO kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |