Moscow
Moscow (Kirusi: Москва - Moskva) ni mji mkuu wa Urusi. Ina wakazi milioni 10.5 na hivyo ni mji mkubwa wa Ulaya.
Jiografia
haririIko katika sehemu ya kiulaya ya Urusi kwa 55°75'N na 37°62'E. Eneo lake ni kwa kimo cha 156 m juu ya UB. Mazingira ni ya vilima vidogo kando la mto Moskva unaobeba maji yake kwa mto Okra unaoishia katika Volga.
Historia
haririMji ulianzishwa mwaka mnamo 1147. Kuanzia 1326 ilikuwa kitovu cha utemi wa kujitegemea. Watemi wa Moscow waliendelea kuwa watawala wa maeneo makubwa zaidi hadi kusimamia Urusi wote. Iwan III. alimwoa binti kutoka familia ya makaisari wa Bizanti na baada ya Bizanti kutwaliwa na Waturuki Moscow ilijaribu kuchukua nafasi yake kama mji mkuu wa Ukristo wa Kiorthodoksi ("Roma ya Tatu").
Mwaka 1703 mji mkuu wa Urusi ulihamishwa kwenda Sankt Petersburg. Baada ya mapinduzi ya kikomunisti mwaka 1918 serikali ikarudi Moscow iliyokuwa tena mji mkuu na kubaki hivyo.
Utamaduni
haririJengo kuu la Moscow ni boma la Kremlin (Кремль) lenye makanisa na majengo mengine mazuri pamoja na makumbusho muhimu. Nje ya Kremlin uko uwanja mwekundu ambao ni uwanja mkubwa mjini unaotumiwa kwa ajili ya maandamano na paredi.
Makumbusho ya Moscow yanasifiwa kote duniani. Pia nyumba zake za maigizo na taasisi za sanaa zinajulikana kimataifa.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Moscow kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |