MS Oasis of the Seas

MS Oasis of the Seas ni meli ya abiria kubwa inayomilikiwa na kampuni kwenye visiwa vya Bahamas. Wakati wa kutengeneywa kwenze mwaka 2010 ilikuwa ni meli kubwa ya abiria duniani.

Meli hii ina uwezo wa kubeba abiria mara tano zaidi ya meli mashuhuri "Titanic" iliyozama kwenye mwaka 1912 baada ya kugongwa na siwa barafu. Tofauti na meli za abiria za zamani zilizosafirisha watu kutoka bandari moja kwenda nyingine Oasis of the Sea sawa na meli za abiria za kisasa inafanya hasa kazi ya burudani ikibeba watalii wanaopenda kuona mabandari na visiwa katika nchi za kigeni.

Meli hii inasadikika kuwa na mambo yafuatayo:

  • 1. hoteli za kifahari zipatazo 69, hoteli hizo zina uwezo wa kupakia vyakula kwa ajili ya wateja wake kwa muda wa siku zipatazo tatu [03], jambo ambalo ni la nadra kupata kutokea na kuwapo.
  • 2. gari moshi dogo ([treni]), gari moshi hili lina uwezo wa kutembea, kuzunguka ndani ya meli hiyo na kupunguza msongamano wa hapa na pale ndani ya meli hiyo.
  • 3. meli ndogo 18 za kuokolea (life boat) pamoja na kuwepo kwa ukubwa wa meli hiyo kumezingatia uwepo wa kuyajali maisha ya mwanadamu hivyo kila boti dogo la wokozi lina uwezo wa kuokoa idadi ya abiria 90 hadi 100 bila kuwapo shida na usumbufu wowote ule kujitokeza.
  • 4. viwanja vya aina zote za mpira, ikiwemo mpira wa mguu, wa kikapu, wa pete, n.k.

Picha hariri

  1. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Log3