Content deleted Content added
Tag: 2017 source edit
Mstari 8:
Nafurahi kuona jinsi gani unavyochangia kwetu swwiki. Asante na karibu tena!. Lakini nakuomba sana usiwe haraka kuhamisha makala yaliyopo. Ile ya chansela-kansela labda haikuwa busara. Hujaonyesha sababu kwa nini unataka kuhamisha makala. Hapa lazima kutafakari pamoja, hasa kwa sababu lemma hii imeshatumiwa mara nyingi. Halafu ni LAZIMA uwasiliane na wengine. Uliulizwa swali kuhusu uhamisho huu na mwenzetu. Desturi kwetu ni ya kwamba tunajitahidi kupeana majibu. Kwa hiyo usikae kimya. Hasa ukiwa mgeni bado ni lazima kuwasiliana na wengine ili tupate kushauriana na kusaidiana. Ukiwa mgeni ni vema kuuliza swali kwanza na kutaja pendekezo na kueleza sababu zako. Usipopata jibu kwa siku kadhaa si kosa kuendelea. '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 19:10, 27 Machi 2018 (UTC)
:Nakubali ilikuwa makosa kuhamisha kwa haraka. Wakati nilitambua kwamba ukurasa huo ulikuwa umeunganishwa na kurasa nyingine mingi, nilijaribu kusuluhisha kwa kutengeneza ukurasa wa 'maana'. Kuhusu swali, nilieleza sababu ya kuhamisha katika muhtasari. Baadaye nikagundua swali lililokuwa limeulizwa mbeleni katika sehemu ya majadiliano. Nashukuru mawaidha yako. Nitatilia maanani siku zijazo na kutathmini hatua kabla ya kutenda. '''[[Mtumiaji:Unja1234|Unja1234]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Unja1234#top|majadiliano]])''' 09:12, 28 Machi 2018 (UTC)
 
::Asante kwa jibu. Wakati mwingine inaweza kutosha kutaja sababu kifupi tu kwenye muhtasari. Lakini mara nyingine na safari hii ingekuwa afadhali kusubiri majadiliano, hasa kama lemma imeshatumiwa mara nyingi. Pamoja na haya ukifanya utafiti lemma hii 1) haiko bado katika kamusi sanifu (niliyo nayo), 2) inapatikana kwa google search kwa maumbo yote mawili yaani Chansela na kansela, ingawa kwa sasa "kansela" ziko zaidi. Lakini kwenye maneno yasiyosanifishwa matumizi yanaweza kubadilika mwaka baada ya mwaka. Na hasa kama mifano ya google ni chache (kama hapa) hatuna tkwimu ya kutegemea. Haya yote si msingi imara wa kubadilisha lemma. Katika wikipedia nyingine hapa kuna mara nyingi chanzo cha edit war. Sisi tumefaulu kuepukana nayo kwa miaka yote kwa kuwasiliana kati yetu kwa heshimu. Karibu kwenye ushirikiano! '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 12:55, 28 Machi 2018 (UTC)