Dar es Salaam : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 31:
== Historia ==
{{main|Historia ya Dar es Salaam}}
Jiji hili zamani lilikuwa [[kijiji]] na kuitwa [[Mzizima]]. [[Sultani]] [[Seyyid Majid]] wa [[Zanzibar]] ndiye aliyechagua jina "Dar es Salaam" linalotokana na [[lugha]] ya [[Kiarabu]] '''دار السلام''' (''Dār as-Salām'') lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili ambayo kimatamshi yanafanana kidogo katika lugha ya Kiarabu yaani "dar" (دار = nyumba, makazi) na "bandar" (بندر = bandari). Hadi leo kuna majengo mawili yaliyobaki ya vyanzo hivi ambayo ni [[Boma la Kale, Dar es Salaam|Boma la Kale]] na [[Atiman House|Nyumba ya Atiman House]].
 
Dar es Salaam ilichaguliwa na [[wakoloni]] [[Ujerumani|Wajerumani]] kuwa [[mji mkuu]] wa [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] kwa sababu ya [[bandari asilia]] yenye mdomo mpana wa [[mto Kurasini]]. Hivyo kuanzia mwaka [[1891]] Dar es Salaam ilichukua nafasi ya [[Bagamoyo]] kama [[makao makuu]] ya [[utawala]].