Majadiliano:Jihadi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '==Maana ya kijeshi ya Jihadi== Mabadiliko ya mtumiaji:JJOSY2000 yameleta tokeo lisiloweza kuridhisha. Amebadilisha matini kwa kudai hakuna maana ya kijeshi...'
 
→‎Maana ya kijeshi ya Jihadi: Mabadiliko ya mtumiaji:JJOSY2000 yameleta tokeo lisiloweza kuridhisha
Mstari 1:
==Maana ya kijeshi ya Jihadi==
Mabadiliko ya [[mtumiaji:JJOSY2000]] yameleta tokeo lisiloweza kuridhisha. Amebadilisha matini kwa kudai hakuna maana ya kijeshi ya istilahi hiyo, bila kuleta chanzo kinachothibitisha maelezo yake. Ameingiza chanzo kimoja ("Answering-Christianity.com) kinachosema " ''Jihad doesn't always mean a war or battle. Any mean for spreading Islam and the Truth, or to fight for what is right and condemn what is wrong (such as fighting the bad and helping the oppressed even if they were not Muslims) are considered Jihad''" - sentensi ya ufunguzi hailingani na madai yake kuwa "Katika Qurani neno "jihadi" halina maana ya mapigano ya kijeshi ". Menginevyo ameleta marejeo yote katika matini yanayothibitisha kinyume ya wazo lake. Tokeo ni makala isiyoeleweka. Kwa sababu hiyo nitarudisha mabadiliko yake, ilhali ninampa kwanza nafasi ya kujibu hapa. '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 18:23, 6 Januari 2021 (UTC)
Return to "Jihadi" page.