Utengule/Usongwe : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''{{BASEPAGENAME}}''' ni jina la kata ya Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 4...
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Picha:Utengule Kanisa mnamo 1898.jpg|thumb|250px|Kanisa la Utengule Usongwe mnamo 1898]]
'''{{BASEPAGENAME}}Utengule''' ni jina la kata ya [[Wilaya ya Mbeya Vijijini]] katika [[Mkoa wa Mbeya]], [[Tanzania]]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa [[2002]], kata ina wakazi wapatao 44,135 waishio humo. <ref>{{cite web|url=http://www.tanzania.go.tz/census/census/districts/mbeyarural.htm|title=2002 Population and Housing Census General Report|publisher=Government of [[Tanzania]]|language=en|accessdate=2008-08-21}}</ref>
 
Kijiji cha Utengule iko kilomita 16 kutoka [[Mbeya (mji)|Mbeya mjini]] kupitia [[Mbalizi]]. Kuna kanisa na chuo cha Biblia cha Moravian. Mazingira ya Utengule pana mashamba ya [[kahawa]] na shamba kubwa ambalo ni mali ya Waswisi walioanzisha pia hoteli ya Utengule Country Club.
 
==Historia==
Jina na mahali ni kihistoria; Utengule ilianzishwa na chifu Tovelamahamba Merere II wa Wasangu aliyepaswa kutoka [[Utengule Usangu]] baada ya kushambuliwa mara kwa mara na Wahehe chini ya [[Mkwawa]]. Alijenga Utengule mpya hapa Usafwa kwenye mtelemko wa mlima Mbeya mahali panapotazama bonde la [[mto Songwe]]. Utengule hii ya Merere II ilikuwa mji uliozungukwa na ukuta na sehemu za ukuta huu bado zinasimama kati ya mashamba na nyumba za kijiji. Merere akishirikiana na Wajerumani katika vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe na baada ya kifo cha Mkwawa Merere III alirudi Usangu alipojenga Utengule upya.
 
Kabla ya kuondoka Merere aliwahi kuwakaribisha wamisionari [[Wamoravian]] walioanzisha kituo cha nje ya mji wa Wasangu mwaka 1895 na kituo hiki cha Wamoravian kilikuwa kitovu kipya cha kijiji. Wamoravian walijenga kanisa, shule na karahana walipofundisha mafundi. Jengo la kanisa lipo hadi leo pamoja na chuo cha Biblia kinachosomesha wainjilisti wa [[Kanisa la Moravian kusini magharibi Tanzania]] (KMKMT). Askofu Mwafrika wa kwanza wa KMKMT [[Yohane Wawenza]] alikuwa mwenyeji wa Utengule.
 
==Marejeo==
*{{marejeo}}
*[http://wisecrack.ca/riftvalley-zanzibar.com/club/index.html Tangazo la Utengule Country Club]
 
{{tanzania-geo-stub}}