Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 404:
:Tafsiri ya "succulent plant" si rahisi. Niliona tafsiri kadhaa lakini sizipendi. Ni wazi kwamba wafasiri/wapendekezaji wengi hawafahamu biolojia sana. Sijui kwamba istilahi moja imeshazagaa sana katika shule na vyuo nyingi. Mimi ninapenda "mmea mwenye majani manono". '''[[Mtumiaji:ChriKo|ChriKo]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:ChriKo#top|majadiliano]])''' 20:25, 29 Novemba 2014 (UTC)
::Asante kwa maelezo. makala iliyotafutwa hasa ilikuwa kuhusu '''Aloe vera.''' Hapa sioni tatizo kutumia jina hili la Kilatini maana inatumiwa kwa Kiswahili siku hizi. ila tu kwa maelezo sawa tutumie mshubiri kwa jenasi '''Aloe'''. Kuhsu succulentes sina upendeleo wowote ila ti swali: je "mmea mwenye '''majani''' manono" ni kweli tunachotaka? Si mtaalamu lakini nikiangalia maelezo mimea hii inatunza maji mara nyingi kwenye majani, lakini mengine pia katika shina. Nimeelewa vema? Sasa kama tunatumia lugha inayotaja majani pekee - je tunaweza kuingiza pia mimea inayotunza maji shinani? '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 17:28, 30 Novemba 2014 (UTC)
:::Ndiyo, "Aloe vera" inaweza kuwa kichwa cha makala. Kuhusu "succulents", ukitaka kutumia uhakika kwamba mimea hii ina utomvu mwingi katika majani na mashina, basi sema "mimea wenye utomvu mwingi". Lakini kwa mtazamo mwangu, hakuna tafsiri fupi ambaye inajulisha maana yake kabisa. Kwa hivyo ninapendekeza kuswahilisha (kuna neno kama hili?) istilahi hii: "sukulenti". Maneno mengi yameswahilishwa. '''[[Mtumiaji:ChriKo|ChriKo]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:ChriKo#top|majadiliano]])''' 18:14, 30 Novemba 2014 (UTC)