Mafunzo yaliyosimamiwa

Mafunzo yaliyosimamiwa (kwa Kiingereza: supervised learning au SL kwa kifupi) ni dhana ya kwenye kujifunza kwa mashine inayotumia data zenye lebo, kufundisha algoriti kuainisha au kutabiri matokeo.

Kielelezo kikionyesha mafunzo yaliyosimamiwa kwa ufupi

Data zenye lebo hujumuisha maingizo (kama maandishi, sauti, au picha) na matokeo yao yanayolingana (kama kategoria, lebo, au alama). Lengo la mafunzo yaliyosimamiwa ni kujifunza funguo (kiingereza:function) itakayobadilisha ingizo jipya kwenda matokeo sahihi kulingana na alama na mahusiano iliyojifunza kwenye data za mafunzo.

Mafunzo yaliyosimamiwa yamegawanyika katika kategoria mbili, uainishaji (kwa Kiingereza: classification) na urudishaji au urejeshaji (kwa Kiingereza : regression). Uainishaji ni kazi ya kubadili maingizo kwenda kwenye matokeo yenye thamani za kipekee (kiingereza discrete values), kama kuainisha kama barua pepe ni barua taka au sio barua taka, mbwa au paka, hisia hasi au hisia chanya, kwa maneno mengine, uainishaji hufanya kazi ya kupanga maingizo kwenye makundi maalumu kulingana na mahusiano iliyojifunza kati ya maingizo na matokeo kwenye data za mafunzo. Urudishaji ni kazi ya kubadili maingizo kwenda kwenye matokeo yenye thamani zinazoendeleea, kama bei, umri au joto, kwa maneno mengine, urudishaji hufanya kazi ya kutabiri tokeo jipya kulingana na mahusiano iliyojifunza kati ya maingizo na matokeo kwenye data za mafunzo. [1][2]

Algoriti maarufu za mafunzo yaliyosimamiwa ni pamoja na urejeshaji mstari (kiingereza: linear regression), urejeshaji vifaa (kiingereza: logistic regression), K-nearest neighbors, mashine vekta saidizi (kiingereza: support vector machines) na mtandao wa neva bandia.[3]

Mafunzo yaliyosimamiwa yana matumizi mengi kwenye utambuzi picha (kiingereza: image recognition), usindikaji wa lugha ya asili, utambuzi wa hotuba (kiingereza: speech recognition), uchambuzi wa hisia (kiingereza: sentiment analysis), utambuzi wa ulaghai (kiingereza: fraud detection), na mifumo ya mapendekezo (kiingereza: recommender system).

Mafunzo yaliyosimamiwa ni moja kati ya dhana zinazotumika sana na zilizofanyiwa tafiti nyingi kwenye kujifunza kwa mashine na akili bandia.

Marejeo

hariri
  1. "What is Supervised Learning? | IBM". www.ibm.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-13.
  2. "What is Supervised Learning?". Google Cloud (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-13.
  3. Avikumar Talaviya (2023-03-03). "Top 10 machine learning algorithms with their use-cases". Medium (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-13.
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mafunzo yaliyosimamiwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.