Majadiliano:Autism
Latest comment: miaka 15 iliyopita by Lloffiwr in topic Jina
Jina
haririNi dhahiri kwa Waswahili kutokuwa na ugonjwa huu au tatizo hili. Hivyo si rahisi kuwa na jina? Sijui, ila kwa mujibu wa maelezo ya Kipala anasema "Hali ya Pekee" nami naunga mkono hoja hii, lakini je, jina ni sawa?--Mwanaharakati (Longa) 08:17, 20 Februari 2009 (UTC)
- Kuna kiitu nimesahau. Hata na makala yenyewe inataka masahihisho kwenye sehemu za kutaja ugonjwa (sehemu ya Historia) inahitaji masahihisho na jamii pia!! Binafsi uwezo wangu umeishia hapo.--Mwanaharakati (Longa) 08:20, 20 Februari 2009 (UTC)
- Sijaona jina la Kiswahili. Kamusi ya TUKI inasema kitu kama "Ugonjwa wa akili kwa watoto" lakini hii si sahihi, maana hali inendelea kwa wakubwa. Tena kuna uvutano kama inatakiwa kuitwa ugonjwa au la. Wengine wenye autism wanastawi vizuri wanapata kazi hadi kuwa profesa na kufaulu (ingawa labda si kila kazi wanayoweza) lakini kwa wengine ni kama ulemavu mkali wa akili hawewezi kujisaidia wanamhitaji mlezi. --Kipala (majadiliano) 08:55, 20 Februari 2009 (UTC)
- Pia nilihisi ya kwamba, Waswahili idadi yake ndogo sana ya kuwa na tatizo hili. Na ndiyo maana yamebaki maelezo bila neno kamili. Sasa, toa pendekezo la jina la makala ambalo unahisi litafaa kuita makala hii. Pili, kusahihisha maelezo yaliyoko ndani ya makala! Ni hayo, sijui wewe waonaje.--Mwanaharakati (Longa) 11:36, 20 Februari 2009 (UTC)
- Haya, mwenye anwani hii 91.96.103.100 kabadilisha JAMII. Sijajua ni nani huyo, lakini jambo kubwa ni jina la makala.--Mwanaharakati (Longa) 11:44, 20 Februari 2009 (UTC)
- Tamko rasmi la kupendekeza jina la makala hii bado halijatoka. Sasa tuache jina hilihili ama tututnge la Kiswahili?--Mwanaharakati (Longa) 08:18, 24 Februari 2009 (UTC)
- Kupata jina fupi kwa ajili ya hali hii ni vigumu. Kutumia neno la ulemavu ni bora kuliko ugonjwa. Je, neno la 'maradhi' ina maana gani kamili? Hata tungesema kitu kama 'Ulemavu wa maendeleo ya akili' isingeeleza aina kamili ya ulemavu. Labda ni afadhali kutunga neno jipya kabisa. Lloffiwr (majadiliano) 08:59, 14 Machi 2009 (UTC)