Majadiliano:Chansela (kiongozi)
Si chansela? Kwa nini "ll"? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:07, 21 Machi 2018 (UTC)
Kansela au chansela?
haririYafuatayo yamenakiliwa kutoka Majadiliano_ya_mtumiaji:Unja1234
Nafurahi kuona jinsi gani unavyochangia kwetu swwiki. Asante na karibu tena!. Lakini nakuomba sana usiwe haraka kuhamisha makala yaliyopo. Ile ya chansela-kansela labda haikuwa busara. Hujaonyesha sababu kwa nini unataka kuhamisha makala. Hapa lazima kutafakari pamoja, hasa kwa sababu lemma hii imeshatumiwa mara nyingi. Halafu ni LAZIMA uwasiliane na wengine. Uliulizwa swali kuhusu uhamisho huu na mwenzetu. Desturi kwetu ni ya kwamba tunajitahidi kupeana majibu. Kwa hiyo usikae kimya. Hasa ukiwa mgeni bado ni lazima kuwasiliana na wengine ili tupate kushauriana na kusaidiana. Ukiwa mgeni ni vema kuuliza swali kwanza na kutaja pendekezo na kueleza sababu zako. Usipopata jibu kwa siku kadhaa si kosa kuendelea. Kipala (majadiliano) 19:10, 27 Machi 2018 (UTC)
- Nakubali ilikuwa makosa kuhamisha kwa haraka. Wakati nilitambua kwamba ukurasa huo ulikuwa umeunganishwa na kurasa nyingine mingi, nilijaribu kusuluhisha kwa kutengeneza ukurasa wa 'maana'. Kuhusu swali, nilieleza sababu ya kuhamisha katika muhtasari. Baadaye nikagundua swali lililokuwa limeulizwa mbeleni katika sehemu ya majadiliano. Nashukuru mawaidha yako. Nitatilia maanani siku zijazo na kutathmini hatua kabla ya kutenda. Unja1234 (majadiliano) 09:12, 28 Machi 2018 (UTC)
- Asante kwa jibu. Wakati mwingine inaweza kutosha kutaja sababu kifupi tu kwenye muhtasari. Lakini mara nyingine na safari hii ingekuwa afadhali kusubiri majadiliano, hasa kama lemma imeshatumiwa mara nyingi. Pamoja na haya ukifanya utafiti lemma hii 1) haiko bado katika kamusi sanifu (niliyo nayo), 2) inapatikana kwa google search kwa maumbo yote mawili yaani Chansela na kansela, ingawa kwa sasa "kansela" ziko zaidi. Lakini kwenye maneno yasiyosanifishwa bado matumizi yanaweza kubadilika mwaka baada ya mwaka. Na hasa kama mifano ya google ni chache (kama hapa) hatuna takwimu ya kutegemea. Haya yote si msingi imara wa kubadilisha lemma. Katika wikipedia nyingine hapa kuna mara nyingi chanzo cha "edit war". Sisi tumefaulu kuepukana nayo kwa miaka yote kwa kuwasiliana kati yetu kwa heshima. Karibu kwenye ushirikiano! Kipala (majadiliano) 12:55, 28 Machi 2018 (UTC)
- Nashukuru. Nilikuwa najua tu kuhusu neno 'kansela' pekee kwa vile hutumiwa katika DW.
- Hi si ajabu. DW ni sauti ya Ujerumani. Maana Wa-TZ na Wa-EAK wanaotunga matini za DW-Kiswahili pale Cologne wamejifunza Kijerumani wakitumia neno "Kanzler" au "Kanzlerin" (kike). Hata "chansela" ni utohoaji tu wa neno la Kiingereza. Asili yake ni Kilatini "cancellarius" kwa lugha zote za Ulaya. Ila labda njia ya kupitia Kiingereza itaeleweka rahisi zaidi kwa wasomaji wetu Afrika ya Mshariki. Ni vema kutaja maumbo yote mawili na kutumia redirect. Ninanakili sehemu ya chini kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala tusikie kama wengine wana neno kama ibaki Kansela caadaye kazi kwako kubadilisha makala zote) au irudishwe Chansela.Kipala (majadiliano) 19:40, 28 Machi 2018 (UTC)