Majadiliano:Christopher Richard Mwashinga

Latest comment: miaka 5 iliyopita by Kipala in topic Kujitangaza?

Makala inakosa yaliyomo: tarehe au mwaka wa kuzaliwa, elimu, vitabu alivyoandika, mashairi ya aina gani, kazi yake. Isipoongezwa karibuni ifutwe. Pamoja na hayo sioni ya kwamba mtindo wa Kimarekani kwa kuandika majina XYZ,Jr inafaa hapa. Je babake aliitwa pia Christopher Richard Mwashinga? Na baba huyu ana umaarufu wowote utakaomleta katika kamusi? Kipala (majadiliano) 07:15, 19 Septemba 2011 (UTC)Reply

Hoja haipingiki! Muda tu kabla ya machinjo!--MwanaharakatiLonga 16:37, 19 Septemba 2011 (UTC)Reply
Naona mhariri amejitahidi kuboresha makala siku hadi siku. Imefikia viwango vya maana sasa!--MwanaharakatiLonga 08:53, 30 Septemba 2011 (UTC)Reply

Kujitangaza?

hariri

Bwana Mwashinga, nimeangalia makala yako kwa miaka kadhaa. Naona unajitahidi kuipanusha polepole. Pia kwa kutumia hekima. Hata hivyo, nisipokosei, wachangiaji kama mtumiaji:MaleLiz (tangu 2017), mtumiaji:Londrosi (tangu 2016) na mtumiaji:Richie matadi (tangu 2011, wakati ule bado kwa tahajia ya Kitanzania, baadaye ulijifunza kutumu herufi kubwa) ni wewe mwenyewe. Basi kwenye swwiki tumekuvumulia miaka hii yote, si muhimu sana kusafisha hapa (sijui upande wa enwiki wangesemaje wakiitambua?). Ila tu tumeendelea kidogo. Siku hizi najaribu kukazia utaratibu kuhusu vyanzo. Inaonekana umetumia pesa kiasi kuchapisha vitabu vyako kwenye kampuni ya Maximum Hope Books LLC uliyoanzisha mwaka 2016 (Maximum Hope Books). Ila Tu katika utaratibu wa wikipedia unachofanya ni "self-publishing". Inafaa sana kuionyesha kwenye ukurasa. Je utaionyesha mwenyewe? Kipala (majadiliano) 21:27, 31 Januari 2019 (UTC)Reply

Hello Bro. Kipala. Nimekuelewa. Nashukuru sana kwa mashauri yako ya busara na elimu pia. Ni kweli mpaka sasa vitabu vyangu vya mashairi ya Kiswahili vimechapishwa na kampuni yangu ya uchapishaji iitwayo Maximum Hope Books ambayo inatimiza miaka kumi mwaka huu 2019. Vitabu vyangu vingine vimechapishwa na AuthorHouse. Nitaonesha kwenye ukurasa husika kwamba vitabu hivi vya mashairi ya Kiswahili ni "self-published."
Rudi kwenye ukurasa wa " Christopher Richard Mwashinga ".