Majadiliano:Dini nchini Tanzania

Latest comment: miaka 13 iliyopita by Muddyb Blast Producer

Hizi ripoti za dini za kuziamini sana hasa hiyo ya kuitwa Kamusi Elezo ya Kikristo kwa kusema Tanzania ikifikia mwaka 2050 Wakristo watakuwa 65 na Waislamu asilimia 35. Ina-maana hao Waislamu hawaongezeki ila Wakristo tu ndiyo wanaongezeka? Ndiyo sababu sikupendelea sana kutaja au kudadafua zaidi kuhusu idadi ya wanadini wa Tanzania hasa kwa kufuatia mtindo wenyewe wa nchi yetu. Kwa maelezo yako, ina-maana kwamba sehemu yenye Wakristo wengi, basi hakuna Waislamu hata asilimia moja - wakati hiyo sio kweli. Tazama Moshi mfano kuna Wakristo wengi, lakini wana-msikiti mkubwa kabisa kama jinsi picha inavyoonesha. Takwimu za dini nchini Tanzania bado ni za kinafiki na zipo kisiasa zaidi - hasa ukiangalia mfumo wa uzazi wa Kiislamu na Kikristo ni tofauti kabisaaaaa. Mwislamu mmoja anaweza akawa na wake wawili hadi watatu na hata watoto akawa nao labda kwa mke mmoja watoto wawili, kwa mwingine watatu, na kwa mwingine labda wawili. Je, unajua idadi kamili ya Waislamu walioa wake zaidi ya mmoja? Je, akiwa na mke zaidi ya mmoja unategemea atakosa kuzaa mtoto kwa mwingine angalau na yeye apewe heshima ya umama? Tena kuna wale walioacha wake zao kwa shida za kindoa, wanaoa wake wengine na wake wanaolewa na wame wengine tena wanazaa na kuzaa. Hapo je? Ni afadhali tuasiandikiane habari za kinafiki katika kamusi yetu kwani hao wanaohesabu Wakristo hawahesabbu Waislamu. Cheers.--MwanaharakatiLonga 11:53, 6 Desemba 2010 (UTC) Reply

Naona makala bado haijafikia hali kulingana na kichwa chake kwa sababu "dini nchini TZ" si swali la takwimu tu. Hii ni sehemu moja pekee ya kichwa. Kuhusu dini sioni ubaya kutaja makadirio mbalimbali jinsi yalivyo nitaongeza mengine. Kipala (majadiliano) 16:59, 6 Desemba 2010 (UTC)Reply
Sikiliza, mzee Kipala. Walichokisema hao Wamerekani cha uwongo kwa sababu wao hawajui watu wameongezeka kiasi gani nchini mwetu. Tazama alivyoandika:

The Government does not gather religious identification data in its census as a matter of policy. However, recent information suggests that 62 percent of the population is Christian, 35 percent is Muslim, and 3 percent are members of other religious groups.

Kwa maana hiyo hayo makisio ya namna gani? Haya, ikiwa wanafuata hesabu ya sensa ya mwaka wa 2002, je, wanajua katika familia yangu mimi wameongezeka watu wangapi tangu hapo 2002? Dada'ngu kazaa watoto wengine 2, mtoto wa dada'ngu kazaa 1, mdogo wangu ana 2, na yule dada'ngu aliyefariki mwaka jana kaacha 1. Swali, hawa wote wapo katika famili moja tu, basi. Vipi hizo familia zingine? Hizi ndizo sababu zilizopelekea mpaka uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010 umekuwa na masuala ya kidini na watu wamechukua idadi fake ya Wamerekani na kujipigia matuamaini ya kushinda kwa wingi wa Wakristo waliopo nchini - bila kusahau kwamba kuna Wakristo wengine wanaitaka CCM ila tu Wakatoliki hawaiataki CCM kwa sababu siku hizi haina maslahi nayo. Tena walifikia hadi hatua ya kusema kwamba eti kura za Waislamu zitagawanyika kwa kina Lipumba na vyama vingine na zingine zitakuja kwa Padre wa zamani wa Katoliki (Dr. Wilbroad Slaa) - hivyo basi Kikwete atakuwa hana kura nyingi na nchi tutachukua. Ninasema waziwazi mambo haya yote yanafanywa na Wakatoliki - kwani hatujawahi kusikia Walutheri kwenye vyombo vya habari wakasema eti mchague fulani wala kutoa waraka. Ni afadhali tusitaje za kinafki ikiwa hali halisi watu hawaijui. Mkumbuke kwamba Waislamu si kama Wakristo kwamba wakioa mpaka kufa - kawaida huwa wanaacha na kuoa na kuchwa na kuolewa. Habari ndiyo hiyo.--MwanaharakatiLonga 17:56, 6 Desemba 2010 (UTC)Reply
Mawili: A) kwa jumla hakuna data za hakika. B) Bado watu wanaendelea kuhisi na kukadiria kuanzia wataalamu mbalimbali hadi wanasiasa na mablogger. Hitimosho: tuonyesha data mbalimbali yanyopatikana kwenye intaneti kama mifano ya makadirio yasiyo na hakika.
Sioni faida kutoonyesha kitu. Kama fulani anadai eti 90% ni Wakristo au Waislamu tuitaje kama imepokelewa katika chombo cha habari yenye maana au taarifa ya taasisi rasmi. Jambo hili ni moto kidogo kwa hiyo tuwe wazi. Ila tu ninetetea hapa yooote ni makidirio bila msingi wa uhakika. Kipala (majadiliano) 19:54, 6 Desemba 2010 (UTC)Reply
Haya, soma haya:

KANISA Katoliki Parokia ya Familia Takatifu Jimbo la Sumbawanga, limegoma kuendesha ibada ya maziko kwa marehemu wawili wakidai ibada haitaendelea mpaka pale waumini ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotengwa na kanisa hilo, watakapoondoka ndani ya kanisa hilo.

Marehemu hao ni aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, Mekitrida Maufi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye pia kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Patrick Maufi.

Maiti nyingine ambayo jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ni ya mtoto wa darasa la nne ambaye pia shule aliyokuwa akisoma haijajulikana.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8 mchana na lilidumu kwa saa tatu pale waombolezaji walipoleta miili ya marehemu hao kanisani hapo kwa ibada ya maziko.

Wengi wa waombolezaji hao walikuwa ni wanaCCM wakimsindikiza mfiwa na wengi wao walikuwa wameshatengwa kwa kinachodaiwa kuwa waliisaliti imani yao ya dini wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshabikia mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly

Balaa tupu!--MwanaharakatiLonga 08:41, 14 Desemba 2010 (UTC) Reply

Muddy hata mimi nimesikia habari hizi za Sumbawanga nikashangaa. Sijui ni nini iliyowakojolea kwenye ubongo huko? Ila tu kwa makala hii inasema nini? Kwangu iko wazi kuna udini katika takwimu hii kutoka kila upande hakuna anayejua namba halisi lakini kuna watu kila upande wanaotaka kujivuna wako mbele kabisa. Kwa hiyo sioni njia ila kuweka kandokando makadrio mbalimbali kwa kueleza waziwazi hayana uhakika yote. Hadi utafiti mwenye sifa za kitaalamu unafanywa. Unaonaje? Kipala (majadiliano) 11:07, 14 Desemba 2010 (UTC)Reply
Bwana we acha tu, mzee wangu. Tumeingia katika shida kubwa sasa hivi. Hii itanifanya niamini zile hadithi za kwenye ukurasa huu http://www.pacinst.com/terrorists/chapter5/titanic.html kuhusu mbinu za dhehebu fulani katika kuangamiza ulimwengu wetu. Hayo yaliyoelezwa kwenye makala hiyo sijui hata inakuwaje, lakini nina sadiki kwa kiasi kikubwa kutuletea shida nchini kwetu. Kweli tusubiri wataalamu zaidi.--MwanaharakatiLonga 12:14, 14 Desemba 2010 (UTC)Reply
Ndugu Muddy, nimesoma hapa kuhusu kifo cha dada yako mwaka jana. Pole sana! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:50, 22 Desemba 2010 (UTC)Reply
Ahsante ndugu Riccardo!--MwanaharakatiLonga 15:10, 22 Desemba 2010 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Dini nchini Tanzania ".