Majadiliano:Fransisko wa Asizi
Latest comment: miaka 13 iliyopita by Riccardo Riccioni in topic Umbo la makala
Makala ni nzuri na inaeleza safi kabisaa, lakini huyu bwana kazaliwa wapi? Na kama mwaka wa kuzaliwa upo, mbona haukuandikwa mwanzo? Haijafuata taratibu za wiki hii ya Kiswahili, hivyo irekebishwe...--Mwanaharakati 04:48, 7 Januari 2008 (UTC)
Umbo la makala
haririRicardo amerudisha umbo la makala "Fransisko wa Asizi" jinsi ilivyokuwa awali. Umbo hili si kawaida katika wikipedia na hasa haifai kwa makala ndefu. Maana yake jinsi alivyoandika inazuia kutokea kwa orodha ya yaliyomo. Orodha hii inatakiwa ni msaada. Naomba atafakari haya. Akiona sababu ya kuacha umbo jinsi ilivyo tafadhali atueleze. Nitasubiri nisiposikia kitu nitarudisha mabadiliko niliyoingiza awali. --Kipala (majadiliano) 10:42, 14 Mei 2008 (UTC)
- Basi naona amesharudisha makala tayari umbo lililotakiwa. --Kipala (majadiliano) 17:17, 14 Mei 2008 (UTC)
- Mzee Ricardo tusivutane maana ni mtu wa kabila lako si langu, ila tu jinsi unavyosisitiza kwelikweli anaheshimiwa pia nje ya kanisa katoliki, kwa hiyo nivumulie. Kama Wakatoliki katika TZ wamezoea kutafsiri jina lake kama "Yohane" badala ya "Giovanni" sina neno lakini hapa wikipedia anapaswa kuitwa "Giovanni" kama jina la ubatizo maana wazazi wake kwa bahati mbaya hawakujua bado ya kwamba baada ya karne kadhaa atapendwa hadi Waswahili. Hii ni sababu walimwita "Giovanni" sio "Yohane". Sijui kwako cheo cha "shemasi" ni muhimu namna gani, sijawahi kusikia ya kwamba Wakatoliki wenzangu Wajerumani wamemwita hivyo. Nilibadilisha chanzo hasa kwa sababu haikuwa sawa ya kwamba alikuwa "shemasi aliyeanzisha utawa" maana alianzisha jumuiya na cheo kilifuata baadaye (hata kama labda kwa sheria ya kanisa shirika halikuwahi kutambuliwa bado, hii sikuweza kuchungulia - ila tu una habari ya kwamba alijali cheo hiki???). Naona mambo mengine kadhaa katika makala lakini tusivutane... Ndimi wako kwa heshima! Kipala (majadiliano) 21:00, 17 Juni 2011 (UTC)
- Basi naona amesharudisha makala tayari umbo lililotakiwa. --Kipala (majadiliano) 17:17, 14 Mei 2008 (UTC)
- Samahani, sina nia ya kuvutana juu ya mtu wa amani kama Fransisko, ingawa katika historia amesababisha mabishano mengi... Mimi ni mfuasi wake wa dhati. Ukitaka kuandika Giovanni, mimi naelewa kwamba ni Yohane kwa Kiswahili. Mbona majina mengi tunayatafsiri katika Kiingereza na katika lugha nyingine? Hata Francesco tunasema Fransisko, tukifuata matamshi wa Kihispania na spelling ya Kiswahili! Somo la akina Giovanni huko Italia ni hasa Mbatizaji, si Mtume. Lakini wachache wanaitwa Giovanni Battista. Kuhusu Fransisko sijawahi kusikia hivyo hata mara moja. Kuhusu Bernardone wakati wa Fransisko ubini ulikuwa haujawa jambo la kawaida na la lazima. Ndiyo sababu tunataja baba na babu yake. Kuhusu ushemasi wake, wachache wanakanusha, lakini kwa wengi suala ni kwamba daraja hiyo ilififia kwa karne nyingi, lakini sasa inatiwa maanani tena. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 03:52, 19 Juni 2011 (UTC)