Majadiliano:Graham Payn

Latest comment: miaka 3 iliyopita by Kipala

Makala inajaa lugha isiyoeleweka, kama mtungaji wa kwanza alitumia google translate na kuimwaga bila kusoma tena alichopata. Kipala (majadiliano) 19:53, 24 Juni 2021 (UTC)Reply

Habari ndugu,
Marekebisho yamefanyika, tafadhari pitia kwa mara nyingine. Asante MagoTech Tanzania (majadiliano) 02:33, 26 Juni 2021 (UTC)Reply

NAona pia hakuna vyanzo maana marejeo kwa wikipedia hayakubaliwa hapa. Kipala (majadiliano) 05:13, 25 Juni 2021 (UTC)Reply

Ndugu vyanzo vimerekebishwa, waweza pitia tena. Asante MagoTech Tanzania (majadiliano) 02:34, 26 Juni 2021 (UTC)Reply
Asante, umefanya kazi kubwa. Lakini labda umeona pia kwamba makala za aina hii zinaleta chnagamoto kubwa, maana tukipata mara moja 10 au zaidi za aina hii hatuna watu wa kutosha wanaowekeza muda na nguvu kusahihisha. Tusipoziainisha haraka zitasahauliwa na kubaki. Kadri idadi ya kurasa taka inavyoongezeka, hadhi na thamani ya wikipedia hii itashuka. Kwa hali ya kawaida -jinsi iloivyo katika wikipedia kubwa- makala zinazoonyesha udhaifu na makosa mengi hivi vinaorodheshwa kwenye Fast Delete na kuondolewa hara. Sijui sisi tutaweza kuendelea kuvumilia makala yenye makosa mengi na mabaya kwa muda mrefu tukiziweka katika mchakato wa kupendekeza kufutwa, halafu kutoa nafasi ziangaliwe na wahariri wengine. Kipala (majadiliano) 05:25, 26 Juni 2021 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Graham Payn ".