Majadiliano:Kibonzo

Latest comment: miaka 16 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Kibonzo - Katuni - Komiki

Aliyewahi kuwa mchoraji wa Vikatuni na michoro mingine kwa Afrika ya Mashariki ni John Kaduma ambaye kwa sasa amefariki na anafikirika kuwa bora kwa muda wote. Hadi leo hii Tanzania au Bado hajaja mchoraji kama yeye, na ndiyo maana wamemwita mchoraji bora wa Afrika Mashariki kwa muda wote! Je, hatuwezi kumworodhesha na huyu?--Mwanaharakati (Longa) 06:16, 11 Novemba 2008 (UTC)Reply

Sawa, asante kwa kumkumbuka. Endela tu kumwingiza kwa sababu sijui alipochora kwenye gazeti gani au staili ilikuwaje. Nimemtaja Gado kwa sababu anachora kwenye Daily News ambayo ni -nisipokosei- gazeti linalotoa nakala nyingi katika Afrika ya Mashariki; lakini atajulikana zaidi Kenya si kwenu. Ila tu sijui kama John Kaduma anajulikana upande wa Tanzania tu? --Kipala (majadiliano) 07:56, 11 Novemba 2008 (UTC)Reply
Hapana. Hata Kenya na Uganda pia walimfahamu, kwa sababu alikuwa ndiyo mwanzilishi wa Jarida la "TABASAMU". Alitunga hadithi nyingi hakuna mfano! Hapa una weza kujua zaidi kuhusiana na historia ya waandikaji vitakatuni wa Tanzania, naye Kaduma kaorodheshwa katika moja kati ya watu hao.--Mwanaharakati (Longa) 09:55, 11 Novemba 2008 (UTC)Reply

Kibonzo - Katuni - Komiki

hariri

Nimekuta maneno haya matatu yakitumiwa kwenye kamusi (kibonzo-katuni) na pia mtandaoni (komiki). Sasa kwa Kiingereza watu hutofautisha "cartoon" - ambayo ni picha moja na "comics/ comic strip" ambayo ni hadithi inayosimuliwa kwa picha mfululizo (yaani zaidi ya moja). Sasa sina uhakika kama "kibonzo" kinaunganisha pande zote mbili au ni zaidi "cartoon". Vilevile sina uhakika kama "katuni" ni sawa na Kiing. "cartoon" au inajumlisha pia maana ya "comics". Je nani anaweza kusaidia? --Kipala (majadiliano) 12:19, 11 Novemba 2008 (UTC)Reply

Katuni na Kibonzo jibu lake tusha pata. Lakini ngoja nijaribu na hii "komiki". Nikiangalia mfano wa mfululizo wa hadithi za Marvel Comics, kama vile Spider Man, Fantastic Four, Iron Man na nyingine nyingi. Nikifuata mfululizo huo napata picha ya kuwa "Komiki" ni katuni zenye maajabu, yaani wengi huwa wanapaa au watu waajabu, ikiwezekana hata kuwa jitu kuubwa! Katuni ni katuni tu, ila kuna hizo katuni strip (za michoro) na animation katuni (ambazo zinajumlishiwa sauti na kutembea!). Na mara nyingi wakisema comic film, basi ujue humo lazima kuwe na mambo ya kujump-jump kama superman! Natumai nimejaribu kuelezea kile ninachokifahamu kuhusiana na "komiki". Basi ni hayo tu! Je, kwa upande wako waonaje?--Mwanaharakati (Longa) 05:52, 13 Novemba 2008 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Kibonzo ".