Majadiliano:Klara wa Asizi

Latest comment: miaka 16 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Baadya kufa kwa Fransiko

Mpangilio wa makala

hariri

Salaaam! Kuna tatizo la kupanga makala kwa kutumia vichwa vya habari. Makala yako ya Klara iko safi, kuanzaia maelezo yake hadi mwisho wa makala. Lakini bado ni ndefu na hata haijawekewa vichwa vya habari ili mtu akitaka kusoma habari aliyoiona inamfaa kwake iwe rahisi. Lbda nikupe mfano mmoja uliotakao faa kwa baadaye:

Klara wa Asizi (1193-1253) ni mwanamke wa kwanza kujiunga na tapo la toba la Fransisko wa Asizi tena ni mwanamke wa kwanza kutunga kanuni ya kitawa. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu na msimamizi wa televisheni.

Kuanzia karne XI wanawake wa Ulaya walishika nafasi za maana kuliko kawaida katika jamii na Kanisa, wakijitokeza pia kwa wingi kufuata tapo lolote la kiroho la Kikatoliki au la kizushi. Kumbe Fransisko hakupata mwanamke yeyote wa kumfuata kwa walau miaka sita tangu aongoke, na hata baada ya kumpata Klara, hakuwapata tena wengi. Sababu ni kwamba hakuwa mchungaji wa roho bali mtu mwenye kutafuta njia yake, wala hakuwa na mpango wa kuanzisha lolote, bali alitaka kushiriki tu hali ya watu wa mwisho. Basi, kwa wanawake nafasi ya mwisho haikuwa tu ile ya wakoma, bali pia ya makahaba na ya wachawi. Hivyo kwao chaguo la nafasi ya mwisho lilikuwa gumu zaidi, sio tu upande wa mateso bali pia upande wa dharau, mbali ya kwamba lingesababisha masingizio juu ya uhusiano wao na ndugu wa kiume.

Maisha yake

hariri

Klara alizaliwa mwaka 1193 au 1194, hivyo alikuwa na miaka 12-13 Fransisko alipovua utu wa kale mbele ya mji mzima katika uwanda ule ambako iko nyumba ya Klara. Kwa hakika huyo akaendelea kusikia habari mbalimbali juu ya Fransisko: alivyopata wafuasi, mmojawao Rufino binamu wa Klara; alivyokubaliwa na Papa n.k. Hatujui kama ni kwa sababu hizo kwamba alikataa ndoa mbalimbali mpaka akafikia umri wa miaka 18, wala hatujui kama walikutana mara nyingi kwa mashauri ya kiroho. Ila tunajua kwa hakika kuwa baada ya Klara kukimbia nyumbani usiku na kujiunga na jamaa ya ndugu wadogo, akifuatwa na mdogo wake Agnesi baada ya wiki mbili tu, Fransisko alitimiza wajibu wa kumlisha kiroho kwa mahubiri, mifano na hata maandishi.

Kwa ushahidi wa Klara tunajua kwamba hata kwake himizo kuu la Fransisko lilikuwa kuambatana moja kwa moja na ufukara wa Mwana wa Mungu. Mapema sana (kabla ya mwanzo wa mwaka 1213) Fransisko aliwaahidia akina Klara kuwashughulikia sawa na ndugu wa kiume, akafanya hivyo mpaka kufa, ingawa kipindi fulani alijizuia asiwatembelee kusudi ndugu wengine wasipate kisingizio cha kufanya hivyo.

Shughuli za Kitakatifu

hariri

Klara aliitikia kwa namna bora ya upendo na uaminifu, akamsaidia kuelewa vizuri zaidi wito wake wa kitume. Kufika kwake kwenyewe kulimfanya Fransisko afikirie sana na kushauriana naye juu ya maisha atakayoyashika. Mara wakatambua njia ya wanawake iwe tofauti na ile ya wanaume: kwa hiyo Klara akawa mmonaki na baadaye abesi, ingawa kwa kushika kikamilifu ufukara mkuu na kuhusiana kidugu na wenzake.

Tofauti na ndugu wadogo, ambao Fransisko aliwaelekeza wafuate “mtindo wa Injili takatifu”, yaani Yesu alivyowaagiza mitume waende (Math.10:5-15), aliwaelekeza Waklara kwenye “ukamilifu wa Injili takatifu”, unaoonyeshwa hasa na heri nane na hotuba nzima ya mlimani (Math. 5:1-7:27), bila ya kuwabana kwa mtindo huo wenye vipengele vingi vya pekee. Tofauti inaonekana wazi katika ushahidi wa Askofu Yakobo wa Vitry ulioandikwa mwaka 1216 ukieleza maisha ya Wafransisko yalivyokuwa bado mwanzoni: wote walikuwa wanakula jasho lao, ila ndugu wa kiume kwa kufanya kazi hasa mjini au vijijini, kumbe akina dada kwa kubaki katika makao yao.

Fransisko aliwahurumia daima wanawake hao waliokubali dharau na magumu ya kila aina. Yeye, ambaye hakusita hata kidogo kufuata tu mtindo wa Injili, katika kuwaongoza alizingatia sana udhaifu wa jinsia yao, na kama kwa kulazimishwa tu na Klara alimruhusu kushika magumu mengi: kila mara huruma ya Fransisko na msimamo imara wa Klara vilikutana katika kumpendeza Mungu. Ni baada tu ya kung’amua msimamo huo, kwamba Fransisko alimuahidia atawatunza sawa na ndugu wa kiume. Mwongozo wake wa uso kwa uso ukawa muhimu kuliko kuwaandikia kanuni fulani: badala yake mwenyewe alichukua jukumu la kudumisha ufukara mkuu na udugu katika monasteri ya kike.

Baadya kufa kwa Fransiko

hariri

Baada ya kifo cha Fransisko, akina Klara waliweza kushuhudia madonda ya Yesu katika mikono, miguu na ubavu wa mtakatifu huyo. Halafu wakaendelea kupigania ufukara mkuu dhidi ya mashauri ya watu mbalimbali. Hatimaye Klara alikubaliwa na Papa kanuni mpya iliyofuata ile ya Fransisko kwa kuilinganisha na maisha ya kimonaki ya wanawake hao. Ilikuwa siku moja tu kabla ya kifo chake tarehe 11 Agosti 1253. Alitangazwa mtakatifu mwaka 1255.

Natumai utakuwa kidogo umenipata kuhusiana na kuweka vichwa vya habari katika makala. Hii inasaidia kufanya kurasa kuwa ndefu mno pasipo na mpangilio. Basi kama umeelewa, naomba endelea. Ukiona bado, basi nijulishe!--"Mwanaharakati" (talk) 12:38, 11 Machi 2008 (UTC)Reply

( kichwa cha habari,,nataka kujua juu ya uchangiaji mada na uanzishaji )

hariri

mengi natamani

Rudi kwenye ukurasa wa " Klara wa Asizi ".