Majadiliano:Madola

Latest comment: miezi 7 iliyopita by Kisare in topic Kuanzisha tena majadiliano haya

Sijui kama ni shida kuswahilisha majina ya nchi kwa vile nyingi zinaanza na 'U'. Kwa sasa nimebadilisha hayo tu ambayo ni wazi, tena zile ambazo zimeshaingiziwa makala. Oliver Stegen 01:19, 4 May 2006 (UTC)

Majina ya Kiswahili ya nchi zote yanapatikana mwishoni mwa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI, lakini mengine siyapendi jinsi walivyotohoa. Hata hivyo ni wazi kwamba katika Wiki tunaendelea kuandika majina mengine kwa kufuata Kiingereza bila sababu. Kwa mfano Syria: kwa nini tusiandike Siria au Sirya? Halafu katika ukurasa huu wa Madola mwanzoni imeandikwa mara mbili Marekani kwa maana ya Amerika. Afadhali kuacha Marekani kwa maana ya nchi iliyopo kati ya Kanada na meksiko. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:06, 17 Agosti 2009 (UTC)Reply


Mimi nilitunga sehemu kubwa ya makala za nchi. Kuhusu umbo la majina nilitafakarai muda mrefu maana wakati ule nilikuwa karibu peke yangu. Mwanzoni sikuwa na kamusi toleo la pili ila nilitumia orodha jinsi ilivyoingizwa katika kamusi hai (kamusiproject) walipoonyesha orodha zilizotolewa na Redio Tanzania na TUKI. Niliona udhaifu ya kwamba majina kadhaa zilionekana hafifu yaani walipendelea aina ya pidgin (maandishi ya Kiswahili kutokana na matamshi ya Kiingereza). Hii hata kama umbo la jina hili halikuwa kawaida hata kidogo. Nilijaribu mara kwa mara kupanusha msingi kwa kuchungulia google ("Kwenye XYZ" kwa kupata kurasa za Kiswahili zenye jina hili) na kurasa za Sauti ya China na BBC. Halafu niliweka majina ya kufanana kwa redirect. Tatizo lingine ni ya kwamba orodha ya TUKI in fupi yaani kwa makala ya kijiografia na kihistoria nilipaswa kuamua mwenyewe nitumie umbo gani.

Naomba tuendelee kushauriana. --Kipala (majadiliano) 20:59, 17 Agosti 2009 (UTC)Reply

Nakushukuru kwa kazi yako kama mwasisi. Kama nilivyoandika, mimi pia naona udhaifu wa majina ya TUKI. Si lazima tuifuate moja kwa moja. Lakini baadhi ya majina tunaweza kuirekebisha, hata kama si haraka. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:28, 20 Agosti 2009 (UTC)Reply
Naorodhesha baadhi ya majina yalivyoandikwa katika kamusi na atlasi mbalimbali ili kuchangia mjadala.

Aljeria = Algeria Benini Bukinafaso = Burkina Kameruni Kepuvede Chadi Visiwa vya Ngazija Kodivaa Ginekweta Eritirea Uhabeshi Gaboni Gine Ginebisau Lesoto Bukini Moritania Morisi Nijeri Nijeria Saotome na Prinsipe Senegali Siera Leoni Sudani Uswazi Ushelisheli Ajentina Babadosi Brazili Kanada Kolombia Kostarika Kuba Ekwado Elsavado Jojia Grinlandi Gwatemala Hondurasi Jamaika Meksiko Nikaragwa Paragwai Peruu Santalusia Santavisenti na Grenadini Surinamu Urugwai Afuganistani Azabajani Bahareni Bangladeshi = Bangiladeshi Butani Bara Hindi Irani Iraki Israeli Japani Yordani Kampuchia = Cambodia Kazakistani Kirigizistani Kuwaiti Laosi Lebanoni Malesia Maldiva Myama = Bama Nepali Omani Filipino = Ufilipino Katari Saudia Singapoo = Singapuri Sirilanka Siria Taiwani Tajikistani Tailandi Turukimenistani Uzibekistani Vietinamu = Vietnamu Milki za Kiarabu Yaman Yemeni Kaledonia Mpya Nyuzilandi Visiwa vya Mariana Kaskazini Andora Belarusi Hezegovina Briteni Korasia Saiprasi = Kuprosi Cheki Denmaki Ufini Jibralta Isilandi = Aisilandi Irelandi = Ayalandi Lativia Lishenteni Litwania Lasembagi Masedonia Monako Norwe Polandi Slovena Uswidi = Swideni Ukraini --Riccardo Riccioni (majadiliano) 21:08, 11 Februari 2012 (UTC)Reply

Kuanzisha tena majadiliano haya

hariri

Natarajia kuanzisha tena majadiliano haya. Naelewa wengine hawapendi baadhi ya majina ambayo TUKI imebuni kwa nchi (mimi wala sipendi baadhi). Hata hivyo naamini ni bora tufuate uongozi wa TUKI kwani sisi sio ambao husanifisha Kiswahili. Kunaweza kuwa na majina yasiyofuata TUKI, lakini kwa maoni yangu lazima yawe machache. Mdahalo huu kuhusu majina ya nchi umeshamalizwa na TUKI. Kisare (majadiliano) 07:03, 12 Aprili 2024 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " Madola ".