Majadiliano:Mbuga baridi

Latest comment: miaka 8 iliyopita by Kipala in topic Steppe?

Yafuatayo yamenakiliwa kutoka Majadiliano ya mtumiaji:ChriKo

Steppe? hariri

Salaam, natumaini ulikuwa na Pasaka njema! Siku hizi naangalia Urusi kwa sababu ya mgeni wetu.. Nahitaji neno kwa "steppe". Una ushauri? Mbuga wa manyasi? Pori ya manyasi? Pori manyasi? Porinyasi ? Kipala (majadiliano) 22:55, 7 Aprili 2016 (UTC)Reply

Salaam. Pasaka yetu haikuwa njema kama tulivyopenda kwa sababu mke wangu hajaweza kutembea bado. "Steppe" ni eneo la manyasi bila miti au lenye miti michache na kwa Kiswahili eneo kama hili linaitwa mbuga. Kama eneo likiwa na miti mingi zaidi linaitwa savana. Pori ni istilahi ya jumla au eneo lenye miti na vichaka. Kwa hivyo nadhani kwamba tafsiri nzuri ya "steppe" ni mbuga. ChriKo (majadiliano) 20:14, 8 Aprili 2016 (UTC)Reply
Asante kwa ushauri. Nimesita kutumia "mbuga" maana ni aina ya nchi inayopatikana Afrika. KWANZA Steppe ni aina ya nchi inayopatikana nje tabianchi ya tropiki. Vipi mbuga baridi? PILI nadhani mbuga ni steppe pamoja na aina za savannah, sivyo? Kipala (majadiliano) 19:14, 11 Aprili 2016 (UTC)Reply
Kipala, samahani kwa sababu sinakubaliani na wewe. Kwa maoni yangu ukweli kwamba "steppe" haipatikani hapa Afrika siyo sababu ya kutotumia neno "mbuga". "Steppes" ni aina za "grasslands" na katika sehemu nyingine za dunia zinaitwa "prairy", "cerrado" na "grass savanna". Na "grassland" ni mbuga kwa Kiswahili. Kama "pori" likitumika kumaanisha aina maalumu ya mandhari hili ni eneo lenye vichaka vifupi vyingi (kama "maquis" au "karoo"). Kwa hivyo nadhani kwamba kutumia istilahi mpya "pori ya manyasi" si wazo zuri. Ukitaka tumia "mbuga baridi". ChriKo (majadiliano) 22:04, 15 Aprili 2016 (UTC)Reply
Asante, twende mbuga baridi. Kipala (majadiliano) 14:07, 16 Aprili 2016 (UTC)Reply
Return to "Mbuga baridi" page.