Majadiliano:Namba shufwa na namba witiri
Latest comment: siku 18 zilizopita by Kisare in topic Usawa
Usawa
hariri@Riccardo Riccioni Mambo vipi? Jina la makala hii ni "Usawa". Lakini, makala inahusu dhana ya namba shufwa na namba witiri, ambayo ni tofauti na dhana ya namba iliyo sawa na namba nyingine. Inaonekana tafsiri sisisi ya "parity" katika Kiingereza. Naamini kwamba "Namba shufwa na witiri" au hata "Ushufwa" ingekuwa jina lifaalo zaidi. Kisare (majadiliano) 05:45, 19 Desemba 2024 (UTC)
- @Kisare. Asante kwa kunishirikisha. Mimi nilichangia makala hiyo mara moja tu mwaka 2015. Naona wazo kuu ni "usawa wa kudumu wa idadi ya namba shufwa na zile witiri", ila kichwa hicho ni kirefu mno. Usawa ni kifupi kiasi kwamba kinaweza kisieleweke. Labda "Idadi sare ya shufwa na witiri"? Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:33, 19 Desemba 2024 (UTC)
- Katika hisabati, "parity" haimaanishi idadi sare ya namba shufwa na witiri. Bali, "parity" ni tabia ya kuwa shufwa au witiri. K.m. 4 ni namba shufwa, kwa kuwa inagawanyika kwa 2. "shufwa" ni "parity" yake. Kwa hiyo nadhani "Namba shufwa na witiri" au "Ushufwa" ni jina bora Kisare (majadiliano) 02:20, 21 Desemba 2024 (UTC)