Majadiliano:Nikola Tesla
Kutumika kwa JAMII "Watu wa nchi fulani" kama jamii kuu ya makala, Oliver anasema sio sahihi. Kwa mujibu wa maelezo yake, JAMII Watu wa.. Ni jamii ya chini. Kwa mfano, Wanafizikia wa Serbia, basi jamii yake ya chini inakuwa "Watu wa Serbia". Sijui, ila ninakuu kutoka kwa Oliver. Hivyo jamii hiyo isitumike juu ila itumike kama SUBCATEGORY! Sijui kwa upande wako--Mwanaharakati (Longa) 15:54, 31 Desemba 2008 (UTC)
- Sijaelewa vema. Wewe unaona ni jamii gani inayofaa hapa? Afadhali uweke kiungo kwa mahali pa majadiliano ya Oliver. --Kipala (majadiliano) 13:09, 2 Januari 2009 (UTC)--
Oliver na Mimi
haririSalam nawe!! Ni kweli. Haitoleta picha nzuri kama zingine zitaandikwa Uchina zingine zikaandikwa China. Kuhusu jamii: Mbona uliondoa jamii ya Watu wa Uchina katika makala ya Chow Yun Fat? Au haina haja kuweka jamii hii katika waigizaji au wanamuziki isipokuwa wanasiasa tu? (yaani mwanasiasa pekee ndiyo anastahili kuwekewa jamii ya Watu wa......) Nahitaji kujua.--Mwanaharakati 06:44, 10 Januari 2008 (UTC)
- Mtu mwenye makala ya wikipedia asionekane katika jamii ya chini na vilevile jamii ya juu. Jamii ya Wanamuziki wa ... iko chini ya jamii ya Watu wa ...; sasa tukiwaingiza wanasiasa wote, wanasayansi wote, wanamuziki wote, yaani watu wote katika jamii ya Watu wa nchi fulani, jamii hiyo itajaa mno, tena haitaeleweka vizuri. Sikubagua wanasiasa! Nikimkuta mwanasiasa aliyeingizwa jamii zote mbili Wanasiasa wa ... na tena Watu wa ..., nitamwondoa kutoka katika jamii ya Watu wa nchi yake. Asante kwa swali zuri! --Oliver Stegen 20:25, 10 Januari 2008 (UTC)
Hapo juu kwenye majadiliano chini ya kichwa cha Jamii za watu, Kipala nami tumewahi kuizungumzia mada hiyo. Wasalaam! --Oliver Stegen 20:37, 10 Januari 2008 (UTC)
- Kama hujaelewa nifahamishe. Nitajaribu kuelezea zaidi.--Mwanaharakati (Longa) 13:20, 2 Januari 2009 (UTC)
- Kifupi: jamii ya WATU WA SERBIA itoke hapo usoni. Badala yake itumika kama jamii ya chini ya Wanafiziki wa Serbia. Hapo vipi.--Mwanaharakati (Longa) 13:28, 2 Januari 2009 (UTC)
Sasa nimeelewa. Kimsingi nakubali. Lakini... Naona kama ni nchi ambako hatuna mambo mengi labda ni afadhali kuweka watu wote pamoja? Yaani kwa Serbia hadi sasa hatuna mtu isipokuwa Tesla. Tusipopata sababu ya kuandika zaidi kuhusu mambo ya Serbia anaweza kubaki kwa muda mtu wa pekee. Kumficha tena katika jamii? Faida ya jamii za chini ni ya kwamba hatuna orodha ndefu mno; pia: tunaweza kumkuta mtu kwenye nchi na pia kwenye kazi yake. Ila tu kama makala ziko chache sana haisaidii nikiona tu jamii 6 na kila jamii ina makala moja ndani yake. Heri kuona makala sita zote za Serbia ukurasa pamoja. Hii ni hoja langu lakini nalubali pia mtindo mwingine. Tuwasiliane kwenye ukurasa wa jumuiya? --Kipala (majadiliano) 16:53, 2 Januari 2009 (UTC)
- Naunga mkono hoja yako ya kumweka huyu bwana kwenye jamii ya nchi yake! Ni kweli hawapo wengi kiasi wawe na jamii za chini au jamii enzi. Kwa wakati uliopo ni akheri kuacha hivyo ilivyo, halafu baadaye akipata mwenzake tutamworodhesha kwenye mfululizo wa muundo wa jamii vile unavyotakikana! Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 04:57, 3 Januari 2009 (UTC)