Majadiliano:Nyati-maji wa mwitu

Active discussions

Jina la mnyama huyu kwa KiswahiliEdit

Mimi sina uhakika kuhusu jina la "Nyati-maji wa mwitu". Hata jina kwa Kiingereza linajadiliwa. Angalia Talk:Wild water buffalo.

Rberetta salaam. Jaribio zuri la kwanza! Ningesema tumia majina kama kwa Kiingereza. Kwa hivyo "nyati-maji" awe spishi ya pori au mwitu na "nyati-maji wa kaya" spishi inayofugwa. Lakini watu wengine wanaweza kuwa na mtazamo mwingine, kwa sababu nyati-maji hufikiriwa kuwa spishi ya kaya kwa kawaida. Ile ya mwitu hajulikani sana. Hivi, mnyama huyu anachukuliwa kama spishi, si nususpishi. ChriKo (majadiliano) 00:00, 21 Novemba 2014 (UTC)
ChriKo salaam - Asante kwa shauri yako. Nimesoma makala mengi kujaribu kujibu swali la "spishi au nususpishi". Bado sijui jibu la sahihi.
Kwa hiyo, sijui la kufanya. Nilifikiri ITIS huwa na taarifa ya sasa kabisa, lakini aya ya "comments" katika Bubalus bubalis arnee inaonyesha kwamba wao hawajui pia!
Ukinishauri kuchukua nyati-maji wa mwitu kama spishi (kama makala ya Wikipedia ya lugha nyingine) nitafanya hivyo. Rberetta (majadiliano) 01:34, 21 Novemba 2014 (UTC)
Wazungu nyinyi mna mambo hadi raha! Angalau ChriKo umepata mtu wa kuweza kujibizana kwa lugha moja.. Hongereni!--MwanaharakatiLonga 13:54, 21 Novemba 2014 (UTC)
Hi Muddyb. Yes, I am soooooooo happy! Ninafurahi sana. Sasa kuna mtu ambaye ninaweza kuzungumza naye kuhusu wanyama.
Rberetta, kuhusu swali la spishi au nususpishi ningefuata IUCN na Tume ya Kimataifa ya Istilahi za Kizoolojia (if that's how they call it in Swahili). ChriKo (majadiliano) 12:08, 22 Novemba 2014 (UTC)
Kwa bahati mbaya, mimi siye mwanaikolojia, kama wewe - mimi ni mhandisi! Katika kazi hii, mimi ni mhariri na mwanafunzi mzee. Kama tungezungumza kuhusu biolojia, naogopa ungechoshwa na mimi. :) Lakini, nisingeweza kuchangia kazi hii bila mtaalamu kunisaidia kidogo na kuchungua mchango wangu. Kwa hiyo ninafurahia uwepo wa ChriKo.
Kuhusu spishi au nususpishi, nimeona makala husika ya ICZN. Sasa ni wazi kwamba ICZN imeamua Bubalus arnee ni halali, lakini ITIS haijaikubali bado. Nafikiri jamii ya WikiPedia inafuata mwelekeo wa majina mapya zaidi, bila kujali ITIS. Kwa hiyo, nitabadilisha makala hayo (na kurasa zake za kuelekeza) kutumia Bubalus arnee. Rberetta (majadiliano) 17:41, 22 Novemba 2014 (UTC)
Kuhusu jina la Kiswahili, kama umeandika ChriKo, watu wengi wanafikiri nyati-maji ni mnyama wa kawaida wa kaya. Kwa hiyo, nafikiri lazima tuchague baina ya:
  • Nyati-maji wa mwitu
  • Nyati-maji mwitu (Mimi mwenyewe, napendelea jina hili.)
  • Nyati-maji wa pori
  • Nyati-maji pori
  • Nyati-maji wa Uhindi
  • Arni (Mimi sijawahi kusikia "Arni", lakini ITIS imetaja Arni kama jina moja la huyo mnyama.)
Nilitafuta kwa Google, na niliona watu wengi wanaandika "ng'ombe mwitu" na "mbuzi mwitu" kuliko "~ wa mwitu", "~ pori", au "~ wa pori". Kwa hiyo nafikiri "nyati-maji mwitu" litakuwa jina linalotarajiwa kwa wengi. Rberetta (majadiliano) 17:41, 22 Novemba 2014 (UTC)
Usijali. Hata kama wewe ni mhandisi, naona kwamba unapenda wanyama. Kwa hivyo tutaweza kuzungumzana. Kuhusu jina la Kiswahili, nafikiri kwamba "nyati-maji mwitu" ni ya ovyo kidogo, kwa sababu maji na mwitu ni maneno ya kutambulisha mawili yote. Waswahili wangesemaje? Sijui. ChriKo (majadiliano) 21:42, 22 Novemba 2014 (UTC)
Return to "Nyati-maji wa mwitu" page.