Majadiliano:Blindness (kitabu)
Hongera kwa kazi kubwa ya kutafsiri tena kwa maneno yako mwenyewe! Naomba nitoe shauri kwa sababu bado umbo unahitaji kazi hadi kufikia kiwango cha makala ya kamusi elezo.
- Maandishi marefu vile ni afadhali yakipangwa kwa njia ya vichwa na vichwa vidogo vya ndani (taz. Wikipedia:Mwongozo (Muundo)#Vichwa na vichwa vidogo hasa)
- kuhusu mwanzo wa makala tazama Wikipedia:Mwongozo (Fungasha-na-maelezo zaidi)#Hitimisho: kupanga makala mpya ya wikipedia
- inamsaidia msomaji kuwa na viungo zaidi, kwa mfano kwa lugha, nchi, au majina maarufu ya watu wanaotajwa (taz. Wikipedia:Mwongozo (Viungo vya Wikipedia))
- Viungo muhimu ni jamii (Mwongozo:Jamii) pamoja na interwiki (taz. Mwongozo Interwiki).
- Kuhusu jina la makala tafakarini vema. Yaani Saramago hajaandika kitabu kinachoitwa "Blindness" bali "Ensaio sobre a cegueira". "Blindness" ni jina la toleo la Kiingereza tu. Naona ni chaguo lenu (mtaona watumiaji wengine watasemaje baadaye) kama mnatafsiri jina la kireno kwa Kiswahili au kutumia jina la kireno moja kwa moja. Mkiamua Kiingereza angalau jina la Kireno lifuate mara moja. (Orodha ya interwiki inaweza kusaidia: lugha nyingi zimeamua kutafsiri moja kwa moja kutoka Kireno). "Insha juu ya upofu (riwaya)" ?
- mkiona vema kuna uwezekano kunakili pia Marejo ya Nje kutoka Makala ya Kiingereza (viungo vya Kiingereza havitafsiriwi kama vinalenga vyanzo vya Kiingereza)
- tahajia mtaona wenyewe (maneno 2 yanayokosa nafasi kati yao n.k.) mkirudia kusoma
- mwishowe ni vema kulinanisha na [ya makosa yanayorudia mara kwa mara].
basi haya ilikuwa mengi - nimevutwa na kazi na lugha nzuri naona umbo lilingane! --Kipala (majadiliano) 15:03, 9 Desemba 2009 (UTC)