Majadiliano:Shule

Latest comment: miaka 15 iliyopita by Muddyb Blast Producer

Waungwana, sina uhakika kama ni kweli neno hili linatokana na Kijerumani. Ila kuna babu mmoja kule Uswahilini kwetu alikuwa akitueleza ya kwamba neno Shule na Sekunde yote yanatokana na Kijerumani. Sasa mie sijui kama ni kweli ama namna gani? Naomba uthibitisho kutoka kwenu wakubwa.--Mwanaharakati (Longa) 08:10, 24 Januari 2009 (UTC)Reply

Ni kweli kabisa. Unaona tofauti ukifika Zanzibar - pale utasoma "skuli ya sekondari" maana wameshika umbo la Kiingereza kwa sababu walikuwa chini ya Uingereza tangu mwanzo. Lakini barani kile kitu kilichokuwa kipya ikaja kwa jina la "Schule" kwa Kijerumani na jina hili likapokelewa katika Kiswahili. Nisipokosei ni 1 kati ya maneno mawili ya asili ya Kijerumani yaliyobaki katika matumizi ya kila siku hadi leo na ile nyingine ni "hela". Kwa "sekunde" - inawezekana imepitia Kijerumani pia ila tu ni neno la Kilatini kabisa linalotumiwa katika lugha zote za Ulaya kwa maumbo mbalimbali. Labda ni neno la tatu la asili ya Kijerumani, sijui historia yake katika TZ. Hata "shule" imetoka katika asili ya Kilatini-Kigiriki (Wagermanik wa kale hawakuwa na kitu hiki) lakini umbo la neno la Kiswahili linaonyesha limepitia Kijerumani. --Kipala (majadiliano) 09:06, 24 Januari 2009 (UTC)Reply
Ninashukuru kwa maelezo yako marefu na yenye kutoa mwangaza mwema wa elimu ya asili ya neno la "Shule!" Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 11:20, 24 Januari 2009 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Shule ".