Majadiliano:Tiger
Latest comment: miaka 13 iliyopita by Kipala
Nimerejesha uhamisho wa makala hii kwenda "Namiri" uliofanywa na mtumiaji:NyotayaMagharibi. Kama jina la Kiswahili lipo nakubali kabisa ya kwamba tunapaswa kuitumia. Lakini neno "namiri" sijui, sijaikuta, tena nina wasiwasi ya kimsingi kama inaweza kuwa kweli maana katika mazingira ya Waswahili wanyama hao hawako kabisa. Kama Nyotaya Magharibi au mtumiaji yeyote ana sababu kwa uhamisho huu naomba kuzieleza kwanza hapa kwenye ukurasa wa majadiliano. Sina neno kukubali uhamisho kama sababu zinazoeleweka ziko. --Kipala (majadiliano) 16:01, 29 Machi 2011 (UTC)
- Nakubali na wewe kabisa. Nawaza kwamba "namiri" inatoka Kiarabu, lakini نمر inamaanisha chui. "Tiger" ni ببر (babr) kwa Kiarabu. Ukitaka jina kwa Kiswahili, chagua chui milia. ChriKo (majadiliano) 23:14, 29 Machi 2011 (UTC)
- Naona ni kweli. Asante kwa kudokeza maneno ya Kiarabu.--Kipala (majadiliano) 16:57, 30 Machi 2011 (UTC)