Majadiliano:Usanisinuru

Latest comment: miaka 5 iliyopita by Riccardo Riccioni in topic Tahajia mbaya

Tahajia mbaya

hariri

Tahajia ya istilahi hii si mzuri, ni "usanidinuru" (pia usanidimwanga). Neno hili linatokanana na kusanidi, yaani "to make, manufacture". ChriKo (majadiliano) 16:40, 27 Desemba 2018 (UTC)Reply

Kumbe. Nilifuata KAST inayosema
KAST: Photosynthesis usanisinuru
Sasa KKS E-Sw ina Synthesis n usanisi. Synthesize vt sanisi; unganisha (maneno). Synthetical adj 1 -a usarsi, synthetic chemistry kemia sanisi.
lakini pia Photo (pref) -synthesis n usanidinuru
Ninavyoona KKS-E-Sw haina msimamo hapa. Maoni yako ina maana, ila tu: je tutafute maoni mengine kabla ya kubadilisha kila kitu? Kipala (majadiliano) 21:52, 27 Desemba 2018 (UTC)Reply
Hmm, inaonekana kama kuna mchanganyiko. Wengine wanasema -sanidi, wengine wanasema -sanisi. Glosbe inaonyesha yote mbili. Ukweli ni wapi au yote mbili ni sawa? ChriKo (majadiliano) 07:07, 28 Desemba 2018 (UTC)Reply
Labda Google inaweza kukata shauri? Usanisinuru lina matokeo 8510, usanidimwanga 1930, usanidinuru 691, usanisimwanga 0. Je? ChriKo (majadiliano) 07:25, 28 Desemba 2018 (UTC)Reply
Google haisaidii hapa. Wakati mwingine ni nzuri kutambua kawaida. Lakini hapa inaakisisha tu chaguo letu kwenye wikipedia. Maana pale tunapoingiza msamiati utasambazwa, kama ni nzuri au la. Kipala (majadiliano) 10:32, 29 Desemba 2018 (UTC)Reply
Hiyo ni kweli bila shaka, lakini sasa, tutaamuaje? Sijali kuacha usanisinuru kama kichwa cha makala hiyo na kuongeza usanidimwanga kama kisawe. ChriKo (majadiliano) 15:34, 29 Desemba 2018 (UTC)Reply
Namuunga mkono ChriKo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:12, 30 Desemba 2018 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Usanisinuru ".