Majadiliano:Utamaduni wa Kiafrika
Latest comment: miaka 15 iliyopita by Kipala
Mchangiaji wa mashindano wa wikipedia ametupia tafsiri ya google.translate bila kujali mno matokeo; hapa tunapata mistari kama "Makala kuu yas: African people and demographics of Africa" na mengine - haikubaliki katika sw:wikipedia. Naona makala inaweza kunyoshwa kama mchangiaji anasoma kimakini wikipedia:Mwongozo na kuitikia ushauri wake. --Kipala (majadiliano) 21:39, 10 Desemba 2009 (UTC)
- Nafurahi kuona makala imeboreka kwelikweli. Bado machache hadi kulingana na masharti ya makala mazuri:
- jina la makala lina kosa ndani yake; ama iwe Utamaduni wa Afrika" au "Tamaduni za Afrika" (hapa mtungaji wa kwanza aamue mwenyewe maana yuko katika mashindano ajaribu kusogeza makala kwenda jina jipya au akiona ugumu atuombe sisi wengine (moja kwa moja kwenye ukurasa wa majadiliano wa Muddy au kwangu au kupitia Jumuiya)
- ni vema kuangalia Jamii:Afrika na kuichungulia huko eti ni jamii ndogo zipi zinazofaa kutajwa badala ya / pamoja na makala za en:wikipedia.
- Pamoja na hayo ingesaidia sana kama makala inaweza kurejelea kurasa zilizopo tayari. (Baada ya kuamua jina la kudumu ni vema pia kuingiza kiungo cha kuelekeza makala hii ndani ya kurasa husika)
- Sentensi ya ufunguzi ungesaidia zaidi kuelewa mada yake kama ingetaja waziwazi ya kwamba kuna lugha ya §utamaduni wa Afrika" lakini hali halisi Afrika ina tamaduni mbalimbali ndani yake. Pia sentensi ya ufunzi jinsi ilivyo inatumia lugha ya wakati uliopita ilhali makala inajadili tamaduni za zamani na za kisasa.
- Lugha bado inahitaji jitihada za kuiswahilisha; maana sentensi kadhaa zinaonyesha asili katika translate.google. Mifano:
- "Watu": sentensi mbili za kwanza hazieleweki.
- mabaki mengi ya majina ya Kiingereza yasiyotafsiriwa na google (Afro-Asiatic n.k. linganisha Lugha za Afrika; "lingua franca", "Pan-African"; "Folklore na dini "
- "vyakula na vinywaji vyake hudhania mivuto ya kienyeji" ??
na mengi mengine. Kwa hiyo naondoa onyo la "umbo" lililoboreshwa na kuweka onyo la "lugha".