Majadiliano:Wilaya za Tanzania 2
Latest comment: miaka 10 iliyopita by Muddyb Blast Producer
Naweza kusaidia nini humu? --MwanaharakatiLonga 10:27, 22 Novemba 2013 (UTC)
- Unaweza sana!Asante kwa kuuliza.
- Nataka sasa kuandaa vigezo vya kata vya wilaya mpya.
- Hatua ya pili itakuwa kusahihisha vigezo vya wilaya vilivyopungukiwa maeneo kwa kuunda wilaya mpya.
- Hatua ya tatu ni kucheki kata zenye majina yanayotokea mahali mbalimbali, ambazo zimetofautishwa kwa mfano Ilembo (Mbeya vijijini) na Ilembo (Mpanda). Kama zimetofautishwa kwa kuongeza jina la wilaya hii inahitaji masahihisho sasa; kama kuna kata mpya yenye jina lililopo tayari ni kuongeza nyongeza kwa yale yaliyopo.
- kazi inayofuata ni masahihisho ya makala zote za kata ambazo A) zilihamishwa wilaya na B) ziliuanzishwa kata mpya. Katika hatua hii natumaini msaada wa bot na Rich Farmbrough alinijibu kama anajua mambo haya. Lakini anahitaji orodha ya wazi iliyoandaliwa ni kata zipi zilizohamishwa au kuanzishwa upya . Labda ingekuwa rahisi zaidi kuchukua hii database ya serikali na kuanzisha makala zote upya lakini sitaki kupoteza habari za kata zilizoongezwa katika miaka tangu tumeunda makala hizi.
- Kwahiyo kazi iko tele. Unaonaje? Tugawane mikoa? Mimi sitapiga mbio kama awali lakini mkoa moja moja inawezekana... Kipala (majadiliano) 17:44, 22 Novemba 2013 (UTC)
- Hakuna neno mzee wangu. Nipe orodha yangu kisha nipige mbio zangu kama "Usain Bolt".--MwanaharakatiLonga 14:06, 23 Novemba 2013 (UTC)
- Kama hutaki kuchagua basi uanze kwa mikoa ya pwani na Tanga, halafu Mtwara. Mimi najaribu kuandaa vigezo vya kata za wilaya, tuone nitafika wapi sasa.
- Halafu swali kuhusu majina. Katika database ya sensa naona wameleta tu majina ya Kiingereza, kama vile Babati District na Babati Town District. Hapa nimeanza kuwabatiza kWa Kiswahili kama zamani "Babati Mjini" na "Babati Vijijini" ingawa kwa Kiingereza mara nyingi hawasemi tena "Rural" kama zamani. Unaonaje? Sawa au la? Kipala (majadiliano) 18:01, 23 Novemba 2013 (UTC)
- Ni sawa. Hujakurupuka hata kidogo. Upo sahihi kabisa. Sasa tunakuja katika suala la kupata information. Wapi zinapatikana?--MwanaharakatiLonga 16:06, 24 Novemba 2013 (UTC)
- Chanzo kipo kwenye ukurasa palepale Wilaya_za_Tanzania_2#Chanzo. Kwa bahati mbaya tovuti ya sensa haikupangwa vizuri sana, kwa kuona kata unapaswa kurudi kwenye Moka na Wilaya mara kwa mara.Nimemaliza (natumaini!) vigezo kwa wilaya zote na majina kufuatana na tovuti ya sensa. Hatuna budi kufuata hatua hizo:
- 1. kufungua kata zote za buluu katika kigezo kipya na kuhakikisha ni kweli mahali pa pale (si mahali pa mkoa au eneo tofauti penye jina hilihili, yaani kuna kata mpya zinazoweza kuwa na jina sawa na kata iliyopo tayaripenginepo)
- 2. wakati huohuo kutafuta kigezo cha wilaya ya (za??) zamani ambako maeneo ya wilaya mpya yamechukuliwa, kulinganisha (maana inawezekana kiungo ni chekundu kwa sababu jina hili lapatikana pamoja na mabano tu!) - hapo kusahihisha kama mabano yanaonyesha jina la wilaya ya zamani - mimi najaribu kuandika mkoa lakini haifai kila mahali
- 3.kuunda makala mpya za kata mpya
- 4. kuunda makala mpya za wilaya mpya.
- 5. sijui kama nimesahau kitu?
- Je tumwulize pia Riccardo? --Kipala (majadiliano) 16:29, 24 Novemba 2013 (UTC)
- Pole kwa kuchelewa kukujibu. Haya, hujasahau kitu. Naona pia si vibaya tukimwomba na yeye aingilie kati kwa vile tayari alishaanza kuandika mikoa mipya. Hivyo basi mchango wake unahitajika kwa hali na mali. Nitaanza pwani mchana wa leo!--MwanaharakatiLonga 04:01, 26 Novemba 2013 (UTC)
- Asante. Naogopa kuna kazi zaidi. Nimechungulia data za sensa. Kumbe kuna kata mpya pia katika wilaya nyingi sio wilaya mpya pekee. Naandaa sasa orodha ya kata zote (kazi ya kuchosha) na hii website ya sensa ni mwendapole. Lakini nimeona inasaidia sana kudownload ile taarifa ya sensa na kukopi jedwali kutoka ile pdf inayopatikana. Kwanza kupakiza kila wilaya katika MS Word (hii inafanya jedwali ya word), baadaye kutoka word jedwali zote pamoja kwenda Excel, na hapa kufuta safu ila zile tatu pekee za namba, majina ya kata pamoja na idadi ya wakazi. Mengine (wanaume, wanawake, namba ya household) sitaki. KATIKA WORD mimi naondoa comma zote kwa sababu Excel yangu ni Kijerumani inafuta "0" zote baada ya comma; hapa ujaribishe wewe kwanza kama comma mwishoni mwa namba zinapotea au la.
- Orodha ya majina ya kata katika Excel naweza kupangilisha kufuatana A-B-C halafu kuikopi kwenda "editor" (kuondoa jedwali) halafu word na kuibadilisha kuwa orodha ya kigezo pamoja na mabano mraba kwa wikipedia. Hapa kuna mbinu ya alama za siri za Word (kama ^p, ^m) sijui kama unajua au la? Inarahisisha kazi sana. Kipala (majadiliano) 05:58, 26 Novemba 2013 (UTC)
- Pole kwa kuchelewa kukujibu. Haya, hujasahau kitu. Naona pia si vibaya tukimwomba na yeye aingilie kati kwa vile tayari alishaanza kuandika mikoa mipya. Hivyo basi mchango wake unahitajika kwa hali na mali. Nitaanza pwani mchana wa leo!--MwanaharakatiLonga 04:01, 26 Novemba 2013 (UTC)
- Salaam. Naona "word" yangu haitaki kubadili PDF kwenda word.. Au nielezee kinyume chake? Yaani, PDF iende word! Hebu nipe kwanza huo uchawi wa Kizungu angalau na mie niutumie huku Afrika. Tena umeona nimeanza na pwani kama tuliahidiana. Ila hata mie haitakuwa kama zamani (kwa vile mambo ya masomo na kazi - ukirudi home mapitio ya uliyoyasoma na kadhalika). Ukitazama utaona makala hizi nimeandika saa nne usiku na kuendelea - hadi nansizia mezani! Haya, niongozee tena katika kurahisisha hii kazi!--MwanaharakatiLonga 03:05, 27 Novemba 2013 (UTC)