Habari, Halima Mhando! Karibu katika Wikipedia ya Kiswahili. Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Kwa sasa tupo wachache. Sana-sana utaniona mimi (Muddyb) na mzee wangu (Kipala) tuliyetayari kukusaidia! Mengineyo: nimeona umeanza kuandika maaneo ya Tanga (sishangai kwa kufuatia jina lako). Lakini pia nina wazo moja kama litafaa kwa upande wako. Siku kadhaa nyuma (mimi na Kipala) tulikuwa tukiandika makala kuhusu kata na maeneo ya Tanga. Je, ungependa kuendeleza na kuongezea maelezo katika kata zile? Ukijiona upo tayari, basi fungua/tazama wilaya uliopo (kwa mfano: Wilaya ya Handeni) utaona chini kuna jedwali lenye orodha ya kata za Wilaya hiyo. Basi ukipenda kuendeleza, nasi tutashukuru! Kumbuka kila Wilaya ina orodha ya kata zilizoanzishwa tayari. Kila la kheri. Nikiwa ninatokea Dar es Salaam, niite Muddyb au,--Mwanaharakati (Longa) 05:57, 15 Aprili 2009 (UTC)Reply

Mwanaharakati awe bureaucrat hariri

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwa kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:23, 28 Mei 2009 (UTC)Reply