Mdude Nyagali au mpaluka said nyagali almaarufu kama mdude alizaliwa 25 augost 1987 katika kijiji cha isongole wilaya ya ileje katika mkoa wa mbeya ambapo sasa ileje ipo katika mkoa wa songwe katika nchi ya tanzania iliyopo africa mashariki. Baba yake mdude alikuwa anaitwa said nyagali alikuwa afisa wa serikali kama mchora ramani wa ardhi na mama yake mdude aliitwa Rusia mbalwe alikuwa mjasiliamali aliyekuwa akijihusisha na biashara ndogondogo, Mwaka 1990 wazazi wa mdude walitengana na mdude aliishi na mama yake pekee mpaka 1999 ambapo mama yake alifariki huko kilando sumbuwanga mkoani rukwa baada ya kuugua ghafla huku akimuacha mdude akiwa darasa la 4.

Baada ya kifo cha mama yake baba yake bwana said nyagali alimtelekeza na alikataa kumuhudumia mwanae kitu kilichomfanya mdude kwenda kuishi kwa wajomba zake.

Mdude alianza shule ya msingi mwaka 1995 katika shule ya mkumbukwa iliyopo ileje na baadaye akahamishiwa shule ya msingi msamba 1 iliyopo wilaya ya mbozi mkoa wa mbeya na sasa mkoa wa songwe nchini tanzania.na kuhitimu shule ya msingi 2002.

Mwaka 2003 mdude alichaguliwa kuendelea na masomo sekondary ambayo baadaye wajomba zake waliokuwa wakimsomesha waliishiwa uwezo kitendo kilichofanya mdude ashindwe kuendelea na masomo ya sekondary na baadaye alielekea lubumbashi kusini mwa nchi ya demokratic republic of congo ambapo alijiunga na chuo cha compyuta Mwaka 2007 alirudi tanzania na mwaka 2008 alijiunga na chama cha siasa cha upinzani cha CHADEMA na mwaka 2010 mdude alikuwa kwenye timu ya kuomba michango ya pesa kwa ajili ya kumsaidia aliyekuwa mgombea ubunge wwa chama cha upinzani cha CHADEMA jimbo la mbozi ambaye alikuwa hajiwezi kiuchumi na kumudu kampeni.

Mwaka 2013 mdude alishtakiwa kwa kosa la uchochezi zidi ya serikali,ilikuwa kesi ya kisiasa na baadaye alihukumiwa kwenda jera miaka mitatu au faini laki 2. Mwaka 2015 mdude aliongoza timu ya kampeni za mgombea ubunge wa chama cha upinzani CHADEMA jimbo la vwawa lililopo mkoa wa songwe kusini kaskazini mwa tanzania,Mdude alikuwa meneja kampeni lakini kutokana na tume ya uchaguzi kutokuwa huru katika nchi ya tanzania msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea ubunge wa chama tawala kuwa ndiye msindi bila hata kujumlisha matokeo ya baadhi ya vituo 72 kati ya 271 ambavyo vilikuwa vinampa ushindi fanuel mkisi ambaye alikuwa mgombea ubunge wa upinzani jimbo la vwawa. Mdude ni kinara wa kukosoa serikali bila uoga pamoja na kwamba amekuwa akitishwa na vyombo vya dola,mdude amekuwa akikosoa utendaji mbovu wa serikali ya chama cha mapinduzi CCM chini ya aliyekuwa rais jekaya kikwete na sasa rais magufuri.Mdude amekuwa akifanya hivyo kwenye majukwaa ya kisiasa pamoja na kwenye mitandao ya kijamii. Mdude amekuwa akipinga kuminywa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa watu kujieleza na kwa kutumia sheria kandamizi ya cyber crime ya 2015 ya serikali ya tanzania. Tarehe 26 augost 2016 Mdude alikamatwa na jeshi la polisi mkoa wa songwe kwa tuhuma za uchochezi zidi ya serikali ya rais magufuri na kuratibu maandamano ya amani yaliyokuwa yameandiliwa na chama cha upinzani cha CHADEMA yaliyopewa jina la UKUTA maana yake ni UMOJA WA KUPAMBANA NA UDIKTETA TANZANIA. Mdude aliingizwa kwenye chumba cha mateso kilichopo kituo cha polisi mkoa wa songwe na kuanza kupigwa na kuteswa huku huku ndugu na jamaa pamoja na mawakili wakizuiliwa kutomuona mdude,Baadaye alisafirishwa kutoka vwawa mkoa wa songwe kwenda dar es salaam bila kumpa huduma za kimatibabu wala chakula chini ya ulinzi mkubwa wa polisi.Baada ya kufikishwa dar es salaam alikabidhiwa kwenye kikosi kimoja cha siri kinachoitwa kikosi kazi au TASK FOCE ambacho kazi yake kinapambana na wanasiasa wa upinzani wanaokosoa serikali ya rais magufuri Baada ya mdude kukabidhiwa kwenye kitengo hicho alipelekwa kwenye nyumba moja ya mateso iliyopo msasani maeneo ya dar es salaam kisha kuvuliwa nguo mbele ya maafisa wa kikosi hicho cha siri wakiwemo wanawake na wanaume huku akishikwa sehemu za siri na wanawake,aliteswa huku akiulizwa kwanini anamkosoa rais kwenye mitandao ya kijamii ususani mtandao wa faceook akitumia majina ya Mdude Chadema Nyagali na Mdude Chadema. Alirudishwa kituo cha osterbay akiwa hoi na baada ya malalamiko ya ndugu na jamaa pamoja na mawakili alifikishwa hospitalini tarehe 30 augost 2016 ambapo alilazwa kwa siku 2. Mdude aliendelea kukaa kizuizini bila kupelekwa mahakamani mpaka mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani Tundu lissu alipotoa tamko kuwa endapo mdude wa wenzake wasipopelekwa mahakamani ndani ya siku 4 basi atalishtaki jeshi la polisi kumshikilia mdude kinyume na sheria,ndipo akafikishwa mahakamani kwa tuhuma za uchochezi baada ya kukaa mahabusu kwa muda wa siku 15 wakati sheria inasema mtuhumiwa kukaa polisi ni saa 24 tu. Kesi hiyo ya uchochezi zidi ya Mdude anatetewa na wakili msomi Boniface Mwabukusi.