Karibu kwenye wikipedia ya Kiswahili! Twamfurahia kila mmoja anayechangia tukielekea kuwa kamusi elezo ya kwanza katika lugha ya Kiswahili. Ukiwa na swali lolote uliza tu! Menginevyo kuna kurasa za msaada wa kuanzisha makala zikiwa na maelezo mazuri. Karibu sana ndugu Ninov! --62.154.201.129 13:52, 2 Desemba 2007 (UTC)

Picha za BaoEdit

Salam ndugu Ninov. Kupakia picha katika Commons ni rahisi sana kama kweli ile picha una haki nayo miliki. Inategemea wewe uliilezea vipi wakati wa kuipakia. Nakuomba ujaribu tena labda watakubali, vile vile wanaangalia sana uandikaji wako katika maelezo ya picha yaani (description au images summary) hilo tu ukiweza kueleza vizuri basi wao hawafanyi chochote kile. Pia ukiwa na kawaida ya kuwaeleza wale Wakabidhi (Adminstrators) juu ya hizo picha ulizo pakia basi hamna hatua yoyote itakayochukuliwa juu ya hizo picha ulizo pakia. Ni hasa Bryan na Dido wenye tabia ya kutubana sisi watumiaji. Basi kila lakheri jaribu tena itakuwa sawa tu. --Mwanaharakati 05:48, 4 Desemba 2007 (UTC)