Ninaitwa Nino Vessella.
Ninaishi Latina, (Italia) karibu na Roma.
Zamani sana nilipata digrii ya lugha ya Kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Napoli. Ninapenda sana lugha ya Kiswahili, lakini nasikitika sana kuona kwamba watanzania wengi wanachafua lugha yao kwa kuingiza ovyo maneno ya Kiingereza bila sababu muhimu.
Pia ninatembelea nchi ya Tanzania kila mwaka: kwa kawaida ninakaa karibu mwezi mmoja wilaya ya Tunduru, lakini niliwahi kukaa Mwanza, Bunda, Arusha, Moshi, Zanzibar, Ifakara, Mtwara, Kilwa, Masasi, Songea na Dar es Salaam.
Ninaweza kutumia lugha ya Kiingereza na Kiesperanto