Majira ya kupuputika majani

Majira ya kupuputika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn)[1] ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kiasi. Kadiri ya umbali na ikweta, mchana unazidi kufa mfupi na usiku kuwa mrefu.

Uzuri wa majani kupuputika katika Green Mountain National Forest.

Pamoja na hayo, miti mingi inaweza ikapotewa na majani yote: ndiyo asili ya jina la majira.

Kwa Kiswahili majira ya namna hiyo pia huitwa masika.

Yanafuata majira ya joto (kwa Kiingereza "Summer") na kutangulia majira ya baridi (kwa Kiingereza "Winter").

Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majira ya kupuputika majani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.